bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 26
Genesis 26
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 27 →
1
Njaa ikaingia katika nchi hiyo kuliko ile njaa ya kwanza iliyokuwako siku za Aburahamu; ndipo, Isaka alipokwenda Gerari kwa Abimeleki, mfalme wa Wafilisti.
2
Ndiko, Bwana alikomtokea na kumwambia: Usitelemke kwenda Misri! Kaa katika nchi, nitakayokuambia!
3
Kaa ugenini katika nchi hii, mimi nitakuwa pamoja na wewe, nikubariki. Kwani wewe nao wa uzao wako nitawapa nchi hizi zote, nikitimize kiapo, nilichomwapia baba yako Aburahamu.
4
Nitawafanya wao wa uzao wako kuwa wengi kama nyota za mbinguni, nazo nchi hizi zote nitawapa wao wa uzao wako, namo katika uazo wako ndimo, mataifa yote ya nchini yatakamobarikiwa,
5
kwa kuwa Aburahamu aliisikia sauti yangu, akayaangalia maneno yangu yapasayo kuangaliwa: maagizo yangu na maongozi yangu na maonyo yangu.
6
Isaka alipokaa Gerari,
7
nao waume wa mahalai hapo walipomwuliza habari ya mkewe, akasema: Huyu ni dada yangu, kwani aliogopa kusema: Ni mke wangu, kwa kwamba: Waume wa mahali hapa wasije kuniua kwa ajili ya Rebeka, kwani ni mzuri wa kumtazama.
8
Alipokwisha kukaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akaona, Isaka alivyomchekesha mkewe.
9
Ndipo, Abimeleki alipomwita Isaka, akasema: Kumbe huyo ni mkeo! Umewezaje kusema: Huyu ni dada yangu? Isaka akamwambia: Ni kwa kuwa nilisema: Nisiuawe kwa ajili yake!
10
Abimeleki akasema: Kwa nini umetufanyizia hivyo? Hili lingekuwa jambo kubwa, mtu wa kwetu akilala na mkeo, nawe ungalitukosesha sana.
11
Kwa hiyo Abimeleki akawatangazia watu wake wote kwamba: Atakayemgusa mtu huyu au mkewe hana budi kuuawa.
12
Isaka alipopanda mbegu katika nchi hiyo, akavuna mia mwaka huo, maana Bwana alimbariki.
13
Akawa mtu mkuu, akaendelea vivyo hivyo kuwa mkuu, mpaka akiwa mkuu kabisa.
14
Akawa na makundi ya mbuzi na kondoo, nayo makundi ya ng'ombe, nao watumwa wengi, kwa hiyo Wafilisti wakamwonea wivu;
15
navyo visima vyote, watumwa wa baba yake walivyovichimbua siku za baba yake Aburahamu, Wafisiti walikuwa wameviziba na kuvijaza mchanga.
16
Naye Abimeleki akamwambia Isaka: Toka kwetu! Kwani umepata nguvu za kutushinda sisi kabisa.
17
Basi, Isaka akatoka huko, akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko.
18
Ndipo, alipovirudia na kuvichimbua tena vile visima vya maji, walivyovichimbua siku zile za baba yake Aburahamu, Wafilisti walivyoviziba, Aburahamu alipokwisha kufa, akaviita majina yaleyale, baba yake aliyoviita.
19
Namo mle bondeni, watumwa wa Isaka walipochimba maji, wakapata kisima chenye maji yarukayo.
20
Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana nao wachungaji wa Isaka kwamba: Maji ni yetu! Ndipo, alipokiita hicho kisima jina lake Eseki (Ukorofi), kwa kuwa walimkorofisha huko.
21
Walipochimbua kisima kingine, wakagombana nao hata kwa ajili yake hicho, akakiita jina lake Sitina (Upingani).
22
Kisha akayavunja mahema yake huko, akachimbua kisima kingine; kwa kuwa hawakugombana naye kwa ajili yake hicho, akakiita jina lake Rehoboti (Papana) akisema: Sasa Bwama ametupanulia, tupate kuenea katika nchi hii.
23
Kisha akatoka huko kwenda kupanda Beri-Seba.
24
Huko Bwana akamtokea usiku uleule, akamwambia: Mimi ni Mungu wa baba yako Aburahamu; usiogope! Kwani mimi niko pamoja na wewe, nikubariki na kuwafanya wao wa uzao wako kuwa wengi kwa ajili ya mtumishi wangu Aburahamu.
25
Ndipo, Isaka alipojenga huko pa kutambikia, akalitambikia Jina la Bwana, akalipiga hema lake huko, nao watumwa wake Isaka wakachimbua huko kisima.
26
Huko Abimeleki na rafiki zake Ahuzati na Pikoli, mkuu wa vikosi, wakamwendea na kutoka Gerari.
27
Isaka akawauliza: Kwa nini mmekuja kwangu ninyi mnaonichukia, mkanifukuza kwenu?
28
Wakasema: Tumeona kwa macho yetu, ya kuwa Bwana yuko pamoja na wewe, kwa hiyo tukasema: Na tufanye maagano na wewe na kuapiana sisi na wewe!
29
Usitufanyie mabaya, kama sisi tusivyokugusa, kama sisi tulivyokufanyia mema tu, tukakuacha, uende zako na kutengemana. Nawe sasa umebarikiwa hivyo na Bwana.
30
Ndipo, alipowafanyia karamu, wakala, wakanywa.
31
Kesho yake wakaamka na mapema, wakaapiana kila mmoja na mwenziwe, kisha Isaka akawasindikiza, wakitoka kwake kwenda zao na kutengemana.
32
Ikawa siku hiyo, wakaja watumwa wake Isaka kumpasha habari za kile kisima, walichokichimbua, wakamwambia: Tumeona maji.
33
Naye akakiita jina lake Siba (Kiapo); kwa sababu hii mji huo unaitwa jina lake Beri-Seba (Kisima cha Kiapo) mpaka siku hii ya leo.
34
Esau alipokuwa mwenye miaka 40 akamwoa Yuditi, binti Mhiti Beri; kisha naye Basimati, binti Mhiti Eloni.
35
Wote wawili wakamtia Isaka naye Rebeka uchungu mwingi rohoni.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50