bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 1
Jeremiah 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 2 →
1
Haya ni maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia aliyekuwa miongoni mwa watambikaji wa Anatoti katika nchi ya Benyamini.
2
Neno la Bwana likamjia siku za Yosia, mfalme wa Yuda, mwana wa Amoni, katika mwaka wa kumi na tatu wa ufalme wake.
3
Likamjia tena siku za Yoyakimu, mfalme wa Yuda, mwana wa Yosia, mpaka mwisho wa mwaka wa kumi na mbili wa Sedekia, mfalme wa Yuda, mwana wa Yosia, kuufikisha mwezi wa tano wa kuhamishwa kwao Wayerusalemu.
4
Neno la Bwana likanijia kwamba:
5
Nilipokuwa sijakutengeneza tumboni mwa mama bado, nilikujua, nawe ulipokuwa hujatoka tumboni, nilikutakasa, nikakupa kuwa mfumbuaji wa mataifa.
6
Nami nikasema: E Bwana Mungu, tazama! Sijui kusema, kwani mimi ni kijana.
7
Bwana akaniambia: Usiseme: Mimi ni kijana! Kwani po pote, nitakapokutuma, utakwenda; nayo yote, nitakayokuagiza, utayasema.
8
Usiwaogope! Kwani mimi niko pamoja na wewe, nikuponye; ndivyo, asemavyo Bwana.
9
Ndipo, Bwana alipoukunjua mkono wake, akakigusa kinywa changu, naye Bwana akaniambia: Hivi ndivyo, ninavyoyatia maneno yangu kinywani mwako.
10
Tazama! Siku hii ya leo nimekupa kuwa mkuu wa mataifa na wa milango ya wafalme, uwe mkuu wa kung'oa na wa kuponda, wa kuangamiza na wa kubomoa, tena wa kujenga na wa kupanda.
11
Neno la Bwana likanijia kwamba: Wewe Yeremia, unaona nini? Nikasema: Mimi ninaona tawi lenye kufunua maua.
12
Bwana akaniambia: Umeona vema, kwani mimi nitayafumbua macho, yalilinde Neno langu, nilitimize.
13
Neno la Bwana likanijia mara ya pili kwamba: Wewe unaona nini? Nikasema: Mimi ninaona chungu chenye maji yanayochemka, nao upande wake wa mbele ulioelekea kaskazini umegeuka.
14
Bwana akaniambia: Upande wa kaskazini ndiko, mabaya yatakakofunuliwa, yawafikie wote wakaao nchini.
15
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Nitazameni! Ninaiita milango yote ya kifalme wakaao upande wa kaskazini. Nao watakuja, waweke kila mmoja wao kiti chake cha kifalme malangoni mwa Yerusalemu na ng'ambo za kuta zote za boma lake liuzungukalo, hata kwenye miji yote ya Yuda.
16
Ndipo, nitakapowatokezea mapatilizo yangu kwa ajili ya ubaya wao wote, kwa kuwa wameniacha wakavukizia miungu mingine, wakatambikia yaliyofanywa na mikono yao.
17
Nawe vifunge viuno vyako! Kisha inuka, kawaambie yote, nitakayokuagiza! Usizistuke nyuso zao, nisije kukustusha nyusoni pao!
18
Tazama! Mimi nimekuweka leo kuwa ngome ya mji na nguzo ya chuma na boma la shaba, nchi zote zishindwe nao wafalme wa Yuda, nao wakuu wao, nao watambikaji wao, nao watu waliomo katika nchi hii.
19
Watapigana na wewe, lakini hawatakuweza, kwani mimi niko pamoja na wewe. Ndivyo, asemavyo Bwana, akuponye.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52