bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 51
Jeremiah 51
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 50
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 52 →
1
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona, nikiinua upepo uangamizao, uujie Babeli nao wakaamo walio wenye mioyo ya kuniinukia.
2
Nitatuma wenye nyungo kwenda Babeli, waupepete, kisha watazichukua mali za nchi, kwani siku ile mbaya watazunguka mjini po pote.
3
Hapo hatakuwako mwenye upindi atakayewapiga mshale, wala hatakuwako mwenye shati ya chuma atakayeweza kuwainukia. Lakini msiwaonee uchungu vijana wake! Ila wao wote wa vikosi vyao watieni mwiko wa kuwapo!
4
Hivyo wataanguka tu katika nchi ya Wakasidi waliopata vidonda, nao waliochomwa watalala huko barabarani.
5
Kwani Isiraeli na Yuda hawakuachwa na Mungu wao aliye Bwana Mwenye vikosi, wawe wajane, ila nchi yao wale ilijaa maovu, waliyomkosea Mtakatifu wa Isiraeli.
6
Kimbieni na kutoka mwake Babeli, kila mtu aiponye roho yake, msinyamazishwe kwa ajili ya manza, walizozikora wao! Kwani hii ndiyo siku ya lipizi ya Bwana, awalipishe matendo yao.
7
Babeli ulikuwa kinyweo cha dhahabu mkononi mwa Bwana kilichozilevya nchi zote; mvinyo yake mataifa yaliinywa, kwa hiyo mataifa yakaingiwa na wazimu.
8
Mara Babeli umeanguka, ukavunjika! Ulilieni! Leteni mafuta ya kwaju kuyatia penye madonda yake! Labda utapona.
9
Tulitaka kuuponya Babeli, lakini haukuponyeka; basi, uacheni, twende kila mtu katika nchi ya kwao! Kwani hukumu yake inafika hata mbinguni, inakwenda juu mpaka kwenye mawingu.
10
Bwana ameyatokeza, ya kuwa mambo yetu yameongoka; njoni, tusimulie Sioni, Bwana Mungu wetu aliyoyafanya.
11
Inoeni mishale! Zishikeni ngao! Bwana ameziinua roho za wafalme wa Wamedi, kwani mawazo yake yameuelekea Babeli, auangamize, kwani hili ndilo lipizi lake Bwana, alilipizie Jumba lake takatifu.
12
Twekeni bendera zielekeazo kuta za Babeli! Malindo yatieni nguvu mkiongeza walinzi na kuweka nao wenye kuvizia! Kwani Bwana aliyoyawaza huyafanya, ayatimize nayo yale, aliyoyasema, ya kuwa atawafanyizia wakaao Babeli.
13
Unakaa penye maji mengi, unavyo vilimbiko, lakini mwisho wako umefika, ndipo hapo palipopimiwa choyo chako.
14
Bwana Mwenye vikosi amejiapia mwenyewe kwamba: Ijapo nimekujaza watu kama nzige, itakuwa, wakuzomee kwa kukushinda.
15
Yeye ndiye aliyeifanya nchi kwa uwezo wake, akausimika ulimwengu kwa werevu wake wa kweli, akazitanda mbingu kwa utambuzi wake.
16
Huvumisha maji mbinguni kwa ngurumo na kupandisha mawingu yatokayo mapeoni kwa nchi, kisha hupiga umeme kwenye mvua na kutoa upepo huko, alikouweka.
17
Ndipo, kila mtu anapopumbaa tu, asijue yatokako, hata kila mfua dhahabu hupatwa na soni kwa ajili ya kinyago chake, kwani alichokitengeneza ni uwongo tu, hata pumzi haimo.
18
Havina maana, ni kazi ya kuchekwa tu; siku vitakapopatilizwa huangamia.
19
Lakini aliye fungu lake Yakobo hafanani navyo, kwani yeye ndiye aliyeyatengeneza yote, naye Isiraeli ni ukoo uliopata fungu kwake; Bwana Mwenye vikosi ni Jina lake.
20
Kweli ulikuwa nyundo yangu, nikakutumia kuwa chombo cha vita; hivyo nikaponda mataifa, nikaangamiza nchi za kifalme kwa kukutumia.
21
Nikaponda farasi pamoja nao waliowapanda kwa kukutumia, nikaponda magari nao walioyapanda kwa kukutumia.
22
Nikaponda waume na wake kwa kukutumia, nikaponda wazee na wana kwa kukutumia, nikaponda wavulana na wasichana kwa kukutumia.
23
Nikaponda wachungaji na makundi yao kwa kukutumia, nikaponda wakulima pamoja na ng'ombe wao wa kulima kwa kukutumia, nikaponda watawala nchi na wakuu kwa kukutumia.
24
Lakini machoni penu nitaulipisha Babeli pamoja nao wote wakaao katika nchi ya Wakasidi mabaya yao yote, waliyoyafanya huko Sioni; ndivyo, asemavyo Bwana.
25
Ndivyo, asemavyo Bwana: Utaniona, nikikujia wewe, mlima uangamizao! Umeziangamiza nchi zote, lakini nimekukunjulia mkono wangu, nikuporomoshe, utoke miambani; nitakugeuza kuwa mlima uliochomwa moto.
26
Hawatachukua kwako mawe ya pembeni wala ya msingi, kwani utakuwa jangwa la kale na kale; ndivyo, asemavyo Bwana.
27
Twekeni bendera katika nchi hii! Pigeni mabaragumu kwa mataifa! Yaeueni mataifa, yaujie! Ziiteni nchi za kifalme za Ararati na za Mini na za Askenazi, ziujie! Wekeni mkuu wa vita, aupige! Pandisheni farasi walio wengi kama nzige wenye manyoya!
28
Yaeueni mataifa, yaujie, wafalme wa Wamedi nao watawala nchi wa kwao nao wakuu wao wote na nchi zote za ufalme wao!
29
Ndipo, nchi itakapotetemeka kwa kustuka, kwani mawazo yake Bwana yameuinukia Babeli kuigeuza nchi ya Babeli kuwa peke yake tu, isikae mtu.
30
Wapiga vita wa Babeli wameacha kwenda vitani, hukaa ngomeni, nguvu zao zimezimia, wakageuka kuwa wanawake; makao yao ya mjini wameyateketeza, makomeo yao yakavunjwa.
31
Mkimbizi anamfuata mkimbizi mwenziwe, vilevile mjumbe anamfuata mjumbe mwenziwe kumpasha mfalme wa Babeli habari, ya kuwa mji wake umetekwa, wakiutokea pande zote;
32
ya kuwa vivuko vyote vimechukuliwa, ya kuwa manyasi ya bwawani yamechomwa moto, kwa hiyo wapiga vita wakaishia ukali.
33
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Binti Babeli anafanana na mahali pa kupigia ngano pakitengenezwa na kupondwa, siku za mavuno zitaujia bado kidogo.
34
Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, amenila, amenitowesha, ameniweka kuwa chombo kitupu, amenimeza kama joka na kulijaza tumbo lake, akanifukuza katika paradiso yetu.
35
Makorofi, waliyonitendea, nayo miili ya watu, waliowaua kwetu, na iujie Babeli! ndivyo, watakavyosema wakaao Sioni; damu, walizozimwaga kwetu, na ziwajie wakaao katika nchi ya Wakasidi! ndivyo, watakavyosema Wayerusalemu.
36
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa hiyo mtaniona, nikiwagombea magomvi yenu, nikiwalipizia malipizi yenu; nitaukausha mto wao mkubwa, navyo visima vyao nitavinyima maji, vipwe.
37
Hivyo Babeli utageuka kuwa machungu ya mabomoko na makao ya mbwa wa mwitu, kwa kustukiwa utazomelewa, kwa kuwa hautakaa mtu.
38
Watanguruma wote pamoja kama simba, wataguna kama simba wachanga.
39
Lakini vichwa vyao vitakapokuwa vinene, ndipo, nitakapowapa vinywaji vyao vya kuwalevya, wapige vigelegele, kisha walale usingizi wa kale na kale, wasiamke tena; ndivyo, asemavyo Bwana.
40
Nitawaangusha kama wana kondoo, wakichinjwa kama madume ya kondoo na ya mbuzi.
41
Kumbe Sesaki umetekwa! Kumbe umechukuliwa uliosifiwa na nchi zote! Kumbe Babeli umegeuka kuwa stusho kwa mataifa!
42
Bahari imepanda kuja Babeli, ukafunikizwa na mawimbi yake yaumukayo.
43
Miji yake ikawa ya kustukiwa kwa kuwa nchi kavu na jangwa, ni nchi isiyokaa mtu ye yote, wala hapapiti mwana wa mtu.
44
Nitampatiliza naye Beli mle Babeli nikitoa kinywani mwake, aliyoyameza, mataifa yasimjie tena mengi na mengi; nazo kuta za boma la Babeli zitaanguka.
45
Tokeni mwake, ninyi mlio ukoo wangu! Kila mtu na aiponye roho yake, asifikiwe na makali yake Bwana yenye moto!
46
Mioyo yenu isizimie kwa woga, mtakapozisikia zile habari zitakazosikilika katika nchi hii, mwaka mmoja ikija habari, mwaka mwingine ikija habari tena, nao ukorofi ukizidi katika nchi hii, kwa kuwa watawala nchi watainukiana.
47
Kwa hiyo mtaona, siku ikija, nitakapovipatiliza vinyago vya Babeli, nchi yake yote ipatwe na soni, kwa kuwa watu wake wote waliouawa wataanguka mlemle mwake.
48
Ndipo, mbingu na nchi navyo vyote vilivyomo vitakapouzomea Babeli, kwani toka kaskazini waangamizaji wataujia; ndivyo, asemavyo Bwana.
49
Babeli nao utaanguka kwa ajili ya Waisiraeli walioanguka wakiuawa, kama walivyoanguka watu wa nchi zote wakiuawa kwa ajili ya Babeli.
50
Ninyi mliozikimbia panga, nendeni tu msisimame! Nako katika nchi za mbali mkumbukeni Bwana! Nao Yerusalemu na uingie mioyoni mwenu!
51
Tuliona soni, tulipotukanwa, nyuso zetu zote zikaiva kabisa, wageni walipopaingia Patakatifu pa Nyumba ya Bwana.
52
Ndivyo, asemavyo Bwana: Kwa hiyo mtaona, siku zikija, nitakapovipatiliza vinyago vyake Babeli; ndipo, wenye kuumizwa watakapopiga kite katika nchi yake yote.
53
Babeli ingawa upande hata mbinguni kujijengea huko juu ngome yenye nguvu, huko nako waangamizaji wataujia; ndivyo, asemavyo Bwana.
54
Sauti za makelele zinasikilika upande wa Babeli na shindo la vunjiko kubwa upande wa nchi ya Wakasidi.
55
Kwani Bwana anauangamiza Babeli na kuzikomesha sauti za makelele yake makuu; mawimbi yanayoujia yanavuma kama maji mengi, sauti za kuumuka kwao zinazidi.
56
Kwani mwangamizaji ameujia Babeli, wapiga vita wake watekwe, pindi zao zivunjwe, kwani Bwana ni Mungu mwenye lipizi, hulipisha, naye hasazi akilipisha.
57
Ndipo, nitakapowalevya wakuu wake na werevu wake wa kweli na watawala nchi wake na wajumbe wake na wapiga vita wake, walale usingizi wa kale na kale, wasiamke tena; ndivyo, asemavyo Mfalme, Bwana Mwenye vikosi ni Jina lake.
58
Ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kuta za boma la Babeli, zingawa ni nene, zitabomolewa mpaka chini, nayo malango yake, yangawa ni marefu, yatateketezwa kwa moto. Koo za watu husumbukia mambo ya bure, nayo makabila hujichokesha kwa ajili ya moto.
59
Hili ndilo neno, mfumbuaji Yeremia alilomwagizia Seraya, mwana wa Neria, mwana wa Masea, alipokwenda Babeli pamoja na mfalme Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa ufalme wake; naye Seraya alikuwa mkuu wa makambi.
60
Yeremia alikuwa ameyaandika hayo mabaya yote yatakayoujia Babeli katika kitabu kimoja, ni hayo maneno yote, Babeli uliyoandikiwa humo.
61
Yeremia akamwambia Seraya: Utakapofika Babeli, jitafutie pafaapo, kisha yasome hayo maneno yote!
62
Ndipo, utakaposema: Wewe Bwana, umepaambia mahali hapa, ya kuwa utapaangamiza, pasiwe mtu wala nyama atakayekaa hapa, kwani patakuwa peke yake tu kale na kale.
63
Utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, ukifungie jiwe, kisha ukitupe katikati katika mto wa Furati
64
ukisema: Hivi ndivyo, Babeli utakavyozama, usioneke tena kwa ajili ya mabaya, mimi nitakayouletea, hata wazimie. Mpaka hapa ni maneno ya Yeremia.
← Chapter 50
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 52 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52