bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 32
Jeremiah 32
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 33 →
1
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwake Bwana katika mwaka wa 10 wa Sedekia, mfalme wa Yuda, ndio mwaka wa 18 wa Nebukadinesari.
2
Ilikuwa hapo, vikosi vya mfalme wa Babeli vilipousonga Yerusalemu; naye mfumbuaji Yeremia alikuwa amefungwa uani penye kifungo kilichokuwa kwenye nyumba ya mfalme wa Yuda.
3
Aliyemfunga ni Sedekia, mfalme wa Yuda, kwa kwamba: Mbona unafumbua kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona, nikiutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli, auteke.
4
Naye Sedekia, mfalme wa Yuda, hatapona mikononi mwa Wakasidi, kwani atatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli, watasemeana kinywa kwa kinywa wakionana macho kwa macho.
5
Atampeleka Sedekia Babeli; ndiko, atakakokuwa, mpaka nitakapomkagua; ndivyo, asemavyo Bwana: Mtakapopigana na Wakasidi hamtafanikiwa.
6
Yeremia akasema: Neno la Bwana limenijia kwamba:
7
Utamwona Hanameli, mwana wa mjomba wako Salumu, akija kwako kukuambia: Jinunulie shamba langu lililoko Anatoti! Kwani wewe unapaswa na kulikomboa, liwe lako.
8
Kisha Hanameli, mwana wa mjomba wangu, akaja kwangu uani penye kifungo, kama Bwana alivyoniambia, akaniambia: Jinunulie shamba langu lililoko Anatoti katika nchi ya Benyamini, kwani inakupasa wewe kuwa nalo kwa kulikomboa. Nikatambua; ya kuwa hili ni lile neno la Bwana.
9
Nikalinunua lile shamba kwake Hanameli, mwana wa mjomba wangu, lililoko Anatoti, nikamlipa fedha, nazo zilikuwa fedha kumi na saba.
10
Nikaliandika katika cheti, nikatia muhuri, kikashuhudiwa na mashahidi, kisha nikampa fedha zake na kuzipima katika mizani.
11
Nikakichukua kile cheti cha ununuzi chenye muhuri kilichoandikwa maagano na maongozi, tena kingine kilicho wazi.
12
Hicho cheti cha ununuzi nikampa Baruku, mwana wa Neria, mwana wa Masea, machoni pake Hanameli, mwana wa mjomba wangu, napo machoni pao mashahidi walioyaandika majina yao katika cheti cha ununuzi napo machoni pao Wayuda wote waliokaa uani penye kifungo.
13
Nikamwagiza Baruku machoni pao hivyo:
14
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Vichukue vyeti hivi, cheti cha ununuzi chenye muhuri nacho cheti hiki kilicho wazi, uvitie katika chombo cha udongo, vipate kukaa siku nyingi.
15
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Nyumba na mashamba na mizabibu itanunuliwa tena katika nchi hii.
16
Nilipokuwa nimekwisha kumpa Baruku, mwana wa Neria, cheti cha ununuzi nikamwomba Bwana kwamba:
17
E Bwana Mungu, tazama, wewe ulizifanya mbingu na nchi kwa uwezo wako mkubwa na kwa mkono wako ukunjukao, hakuna kisichowezekana kwako.
18
Watu maelfu huwahurumia, nazo manza, baba walizozikora, huzilipiza kwa wana wao waliotokea nyuma yao. U Mungu mkuu mwenye nguvu; Bwana Mwenye vikosi ni Jina lako.
19
Mashauri yako ni makuu, matendo yako ni mengi, macho yako hufumbuka, yazione njia zote za wana wa watu, umpe kila mtu yazipasayo njia zake nayo yayapasayo mapato ya matendo yake.
20
Ulifanya vielekezo na vioja katika nchi ya Misri mpaka siku hii ya leo kwa Waisiraeli hata kwa watu wengine, ukajipatia Jina, kama linavyojulikana leo.
21
Walio ukoo wako wa Isiraeli ukawatoa katika nchi ya Misri kwa kufanya vielekezo na vioja kwa kiganja chenye nguvu cha mkono ukunjukao, ukatisha kwa matisho makuu.
22
Ukawapa nchi hii, uliyowaapia baba zao kuwapa, ni nchi ichuruzikayo asali na maziwa.
23
Wakaja, wakaitwaa, kisha hawakuisikia sauti yako, wala hawakuyafuata Maonyo yako, wala hawakuyafanya yote, uliyowaagiza, wayafanye; kwa hiyo umewaletea haya mabaya yote.
24
Tunayaona haya maboma, yako karibu, ni ya kuutekea mji huu; kweli mji huu utatiwa mikononi mwa Wakasidi wanaoupigia vita, maana panga na njaa na magonjwa mabaya yataushinda, yatimie uliyoyasema, nawe utakuwa ukiyatazama tu.
25
Wewe Bwana Mungu, umeniambia: Jinunulie shamba kwa fedha, mashahidi wakiwako kuvishuhudia. Lakini mji huu utatiwa mikononi mwa Wakasidi.
26
Neno la Bwana likamjia Yeremia kwamba:
27
Tazama! Mimi ni Bwana, Mungu wao wote walio wenye miili. Je? Liko lo lote lisilowezekana kwangu?
28
Kwa hiyo Bwana anasema hivi: Mtaniona kweli, nikiutia mji huu mikononi mwao Wakasidi namo mkononi mwake Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, auteke.
29
Kweli Wakasidi wanaoupigia mji huu vita watauingia, watauchoma moto mji huu na kuziteketeza nyumba, walimomvukizia Baali darini juu, nazo zile, walimomwagia miungu mingine vinywaji vya tambiko, kusudi wanikasirishe.
30
Kwani wana wa Isiraeli nao wana wa Yuda tangu ujana wao huyafanya yale tu yaliyokuwa mabaya machoni pangu, kweli wana wa Isiraeli wamenikasirisha kwa matendo ya mikono yao; ndivyo, asemavyo Bwana.
31
Kwani mji huu umenichafua na kuuwakisha moto wa makali yangu kuanzia siku ile, walipoujenga mpaka siku hii ya leo; kwa hiyo ninauondoa usoni pangu
32
kwa ajili ya mabaya yote, wana wa Isiraeli na wana wa Yuda waliyoyafanya, kusudi wanikasirishe, wao wenyewe na wafalme wao na wakuu wao na watambikaji wao na wafumbuaji wao, walio watu wa Yuda nao wakaao Yerusalemu.
33
Wakanigeuzia kosi zao, sizo nyuso; nami naliwafundisha pasipo kuchoka kila kulipokucha, lakini hawakuwako waliosikia, waonyeke.
34
Wakayaweka matapisho yao katika ile Nyumba iliyoitwa kwa Jina langu, waitie uchafu.
35
Wakamjengea Baali pa kumtambikia vilimani juu katika Bonde la Mwana wa Hinomu, wawatumie wana wao wa kiume na wa kike kuwa ng'ombe za tambiko za Moloki, nami sikuwaagiza hivyo, wala havikunijia moyoni, ya kuwa watafanya tapisho kama hilo, kusudi wawakoseshe Wayuda.
36
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema sasa kwa ajili ya mji huu, ambao mnasema, ya kuwa umetiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli kwa nguvu za panga na za njaa na za magonjwa mabaya:
37
Mtaniona, nikiwakusanya na kuwatoa katika nchi zote, nilikowaendesha na kuwakimbiza kwa makali yangu yaliyowaka moto na kwa machafuko makuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwapa kukaa salama.
38
Nao watakuwa ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
39
Nami nitawapa kuwa wenye moyo mmoja washikao njia moja tu, waniogope siku zao zote; hivyo watajipatia mema wenyewe hata wana wao watakaokuwa nyuma yao.
40
Nitafanya nao agano la kale na kale, ya kuwa sitaacha kuwafuata na kuwafanyizia mema, namo mioyoni mwao nitatia woga wa kuniogopa, wasiondoke tena kwangu.
41
Nami nitawafurahia, niwafanyizie mema, kweli nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na kwa roho yangu yote.
42
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kama nilivyowaletea wao wa ukoo huu haya mabaya yote yaliyo makuu, ndivyo, nitakavyowaletea mema yote, niliyowaambia mimi.
43
Mashamba yatanunuliwa tena katika nchi hii, mnayoisema ninyi, ya kuwa ni nyika tu pasipo watu na nyama kwa kutiwa mikononi mwa Wakasidi.
44
Mashamba yatanunuliwa kwa fedha, hata vyeti vya ununuzi vitaandikwa na kutiwa muhuri na kushuhudiwa na mashahidi katika nchi ya Benyamini na pande zote za Yerusalemu, namo katika miji ya Yuda, namo katika miji iliyoko milimani, namo katika miji iliyoko mbugani, namo katika miji iliyoko upande wa kusini; kwani nitayafungua mafungo yao; ndivyo, asemavyo Bwana.
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 33 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52