bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 3
Jeremiah 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 4 →
1
Akasema: Kama mtu anampa mkewe ruhusa, ajiendee, naye akatoka kwake, akawa wa mume mwingine, je? Yule wa kwanza atamrudia? Nchi ile isingepata uchafu? Nawe wewe umezini na wenzio wengi, kisha unirudie mimi! ndivyo, asemavyo Bwana.
2
Yaelekeze macho yako vilimani, utazame! Pako mahali, usipofanyiziwa ugoni? Ulikaa njiani na kuwangoja kama Mwarabu nyikani, ukaichafua nchi kwa ugoni wako uliokuwa mbaya.
3
Kwa hiyo ulinyimwa mvua za masika, hata za vuli hazikunya, lakini paji lako ni lilelile la mwanamke mgoni, ukakataa kuingiwa na soni.
4
Tena unaniita sasa: Baba yangu! Wewe ulikuwa mwenzangu mpendwa wa siku za ujana!
5
Je? Atakasirika siku zote, asiniondolee makosa kale na kale? ndivyo, unavyosema; kisha unayafanya mabaya, unayoyaweza.
6
Bwana akaniambia siku za mfalme Yosia kwamba: Umeyaona, binti Isiraeli aliyoyafanya akiniacha? Alipanda kila kilima kirefu, akakaa chini ya kila mti wenye majani mengi kufanya ugoni palepale.
7
Alipokwisha kuyafanya hayo yote, nimesema: Rudi kwangu! Lakini hakurudi, hata dada yake binti Yuda avunjaye maagano aliyaona.
8
Nikauona huo ugoni wote, alioufanya binti Isiraeli akiniacha, nikampa ruhusa, ajiendee, nikampa nacho cheti cha kuachana. Lakini naye dada yake binti Yuda hakuogopa, akaenda, akafanya ugoni naye.
9
Ikawa, uvumi wa ugoni wake ukaichafua nchi, akazini akitumia mawe na miti.
10
Alipoyafanya hayo yote, naye dada yake binti Yuda avunjaye maagano hakurudi kwangu kwa moyo wake wote, ila kwa uwongo tu; ndivyo, asemavyo Bwana.
11
Bwana akaniambia: Binti Isiraeli akiniacha, roho yake ni njema kuliko yake binti Yuda avunjaye maagano.
12
Nenda kuyatangaza maneno haya na kupaza sauti upande wa kaskazini, useme: Rudi, binti Isiraeli uliyeniacha! ndivyo, asemavyo Bwana: sitawatazama kwa macho makali, kwani ni mpole. Ndivyo, asemavyo Bwana; Sitakasirika kale na kale.
13
Jua tu, ya kuwa umekora manza ulipomtengua Bwana Mungu wako ukienda huko na huko kufuata wageni chini ya kila mti wenye majani mengi, lakini sauti yangu hukuisikia; ndivyo, asemavyo Bwana.
14
Rudini, ninyi wana mlioniacha! ndivyo, asemavyo Bwana. Kwani mimi ni bwana wenu; nitawachukua mmoja katika mji mmoja, tena wawili katika udugu mmoja, niwapeleke Sioni.
15
Nitawapa wachungaji waupendezao moyo wangu, wawachunge, mpate ujuzi wa kuerevuka.
16
Ndivyo, asemavyo Bwana: Hapo, mtakapokuwa wengi kwa kuzaa wana katika nchi ile, siku zile hawatalitaja tena Sanduku la Agano la Bwana, halitaingia moyoni mwa mtu, hawatalikumbuka, hawatataka kuliona, wala hawatafanya jingine tena.
17
Siku zile Yerusalemu watauita Kiti cha kifalme cha Bwana; kule Yerusalemu ndiko, wamizimu wote watakakokusanyikia kwa ajili ya Jina la Bwana, hawataendelea tena kuufuata ugumu wa mioyo yao mibaya.
18
Siku zile mlango wa Yuda utauendea mlango wa Isiraeli, nao watakuja pamoja wakitoka katika nchi ya upande wa kaskazini, waje kuikalia nchi, niliyowapa baba zenu, iwe fungu lao.
19
Nami nalisema: A, nitakuweka kwenye wana, nitakupa nchi ya kupendezwa nayo kwa kuwa yenye utukufu kuyapita matukufu yote ya wamizimu! Nikasema: Utaniita: Baba! Usiondoke nyuma yangu!
20
Lakini kama mwanamke anavyomdanganya mwenziwe akimwacha, ndivyo, mlivyonidanganya na kuniacha, ninyi wa mlango wa Isiraeli; ndivyo, asemavyo Bwana.
21
Sauti zinasikilika vilimani juu, ni kilio cha malalamiko ya wana wa Isiraeli, kwa kuwa wamezipotoa njia zao kwa kumsahau Bwana Mungu wao.
22
Rudini, ninyi wana mlioniacha! Nitawaponya, ingawa mmeniacha. Tutazame! Tumekujia, kwani wewe ndiwe Bwana Mungu wetu.
23
Kweli mambo ya vilimani juu ni ya uwongo tu, nayo michezo ya vileleni milimani; kweli kwake Bwana Mungu wetu ndiko, wokovu wa Isiraeli uliko.
24
Jambo lenye soni limeyala mapato ya baba zetu tangu ujana wetu, kondoo na mbuzi wao na ng'ombe wao, hata wana wao wa kiume na wa kike.
25
Sharti tulale kwa kupatwa na soni, nayo matusi yatufunike, kwani tumemkosea Bwana Mungu wetu, sisi na baba zetu tangu utoto wetu mpaka siku hii ya leo, hatukuisikia sauti ya Bwana Mungu wetu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52