bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 50
Jeremiah 50
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 49
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 51 →
1
Hili ndilo neno, Bwana alilolisema kwa kinywa chake Yeremia kuwaambia Wababeli walioko katika nchi ya Wakasidi.
2
Yatangazeni kwa mataifa, wayasikie! Twekeni bendera! Yasimulieni, msiyafiche! Semeni: Babeli umetekwa, Beli amepatwa na soni, Merodaki amestuka, vinyago vyao vimeumbuliwa, mifano yao imevunjika!
3
Kwani taifa lililotoka upande wa kaskazini limewapandia, hilo limeiharibu nchi yao iwe peke yake, isikae tena wala mtu wala nyama, wamekimbia kwenda zao.
4
Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku zile za wakati huo ndipo, wana wa Isiraeli pamoja na wana wa Yuda watakapokuja wakienda na kulia machozi; hivyo watakwenda kumtafuta Bwana Mungu wao.
5
Watauliza njia ya kwenda Sioni; ndiko, nyuso zao zinakoelekea kwamba: Njoni kuandamana na Bwana, tukifanya agano la kale na kale lisilosahauliwa tena!
6
Walio ukoo wangu walikuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao waliwapoteza, wakatangatanga milimani, walipotoka mlimani wakaendea kilima kingine, wakakisahau kituo chao.
7
Wote waliowaona wakawala, nao waliowasonga wakasema: Hatukosi. Hayo yakawapata, kwa kuwa walimkosea Bwana aliyekuwa lisho lao la kweli, ni yeye Bwana, baba zao waliyomngojea.
8
Kimbieni, mwutoke mji wa Babeli, mliomo! Itokeni nayo nchi ya Wakasidi, mwe kama madume ya kondoo wanaoyatangulia makundi!
9
Kwani mtaniona mimi, nikiinua mkutano wa mataifa makubwa yatokayo upande wa kaskazinni, niyapandishe kwenda Babeli; watakapojipanga, hapohapo ndipo, utakapotekwa. Mishale yao ni kama ya mpiga vita mwerevu asiyerudi mikono mitupu.
10
Nchi ya Wakasidi itatekwa, nao watakaoiteka watashiba wote; ndivyo, asemavyo Bwana.
11
Kwa kuwa mwalifurahi, mkapiga vigelegele hapo, mlipolipokonya fungu langu, mkachezacheza kama ndama wakipura, mkalia kama farasi wenye nguvu:
12
mama yenu atapatwa na soni kabisa, yeye aliyewazaa ataiva uso; hapo mtaona, hilo taifa lililokuwa la mwisho linavyogeuka kuwa nyika kavu na jangwa.
13
Kwa kukasirika kwake Bwana hautakaa mtu, wote pia utakuwa peke yake tu, kila atakayepapita palipokuwa na Babeli, atapastuka na kuuzomea kwa ajili ya mapigo yake yote.
14
Jipangeni na kuuzunguka Babeli, ninyi nyote mpindao pindi! Upigeni mishale, msiitendee choyo! Kwani wamemkosea Mungu.
15
Pigeni vigelegele po pote! Umejitia mikononi mwenu! Maboma yake yamebomolewa, kuta zake zimeangushwa, kwani hili ndilo lipizi la Bwana, kwa hiyo ulipisheni! Kama ulivyofanya, ufanyizieni!
16
Huko Babeli wang'oeni wapanzi nao wavunaji washikao miundu siku za mavuno! Kwa kuzikimbia panga za wenye nguvu kila mtu atawageukia walio wa ukoo wake, kwa hiyo kila mtu ataikimbilia nchi ya kwao.
17
Waisiraeli ni kama kondoo waliotawanyika kwa kufukuzwa na simba: kwanza mfalme wa Asuri aliwala, mwisho Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliwavunja mifupa.
18
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Mtaniona, nikimpatiliza mfalme wa Babeli na nchi yake, kama nilivyompatiliza mfalme wa Asuri.
19
Nitawarudisha Waisiraeli kwao, walikokaa, wajilishe mazao ya Karmeli na ya Basani, roho zao zishibe milimani kwa Efuraimu nako huko Gileadi.
20
Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku zile zitakapotimia, manza, Waisiraeli walizozikora, zitatafutwa, lakini zitakuwa haziko, nayo makosa ya Wayuda, lakini hayataonekana, kwani nitayaondoa kwao, nitakaowasaza.
21
Ipandie nchi yenye makatavu mawili, uingie namo, wakaamo wenye kupatilizwa! Waue na kuwamaliza walio nyuma yao! Yafanye yote, kama nitakavyokuagiza!
22
Sauti za vita zinasikilika katika nchi hii, nayo mavunjiko ni makubwa.
23
Kumbe nyundo iliyozipiga nchi zote imepondeka kwa kuvunjikavunjika! Kumbe Babeli umegeuka kuwa wa kustukiwa na mataifa yote!
24
Nimekutegea, wewe Babeli, ukanaswa, nawe ulikuwa huvijui; umeonwa, ukakamatwa, kwani umemtaka Bwana, mpigane.
25
Bwana amelifungua limbiko lake, akayatoa mata ya makali yake, kwani yeye Bwana Mungu Mwenye vikosi yuko na kazi katika nchi ya Wakasidi.
26
Njoni huku na kutoka kwenye mapeo ya nchi! Vifungueni vyanja vyake vya ngano, mzikusanye kuwa chungu, kisha zimalizeni kwa kuziteketeza, masao yasipatikane kamwe!
27
Wachomeni ng'ombe wao wote kwa mikuki, waanguke kwa kuchinjwa hivyo, Watapatwa na mambo, kwani siku yao inakuja, watakapopatilizwa.
28
Sauti zao walioitoka nchi ya Babeli kwa kukimbia mbio sana zinasikilika Sioni, wakiyatangaza malipizi ya Bwana Mungu wetu, jinsi alivyolilipizia Jumba lake takatifu!
29
Waiteni wapiga mishale wote wanaopinda pindi, waje Babeli, wapige kambi zao kuuzunguka, usipate pa kukimbilia. Ulipisheni matendo yake! Yote, uliyoyafanya, ufanyizieni yaleyale! Kwani umejivuna kuwa mkuu kuliko Bwana, kuliko yeye aliye Mtakatifu wa Isiraeli.
30
Kwa hiyo vijana wako wataangushwa barabarani mwako, nao waume wote wa kupiga vita watanyamazishwa siku hiyo; ndivyo, asemavyo Bwana.
31
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu Mwenye vikosi: Utaniona, nikikujia, wewe mkorofi; kwani itakuja siku yako, nitakapokupatiliza.
32
Ndipo, mkorofi atakapojikwaa, aanguke, lakini hatakuwako atakayemwinua; mijini mwake nitawasha moto, uiteketeze yote pande zake zote.
33
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Wameteseka wana wa Isiraeli pamoja na wana wa Yuda; wote waliowateka na kuwahamisha wanawashika, wakakataa kuwapa ruhusa kwenda.
34
Lakini mkombozi wao ni mwenye nguvu, Bwana Mwenye vikosi ni Jina lake. Yeye atawagombea hayo magomvi yao, kusudi aitulize nchi, lakini wakaao Babeli atawahangaisha.
35
Ndivyo, asemavyo Bwana: Panga na ziwajie Wakasidi nao wakaao Babeli nao wakuu wao nao werevu wao wa kweli!
36
Panga na ziwajie wapuzi, wapumbae! Panga na ziwajie wapiga vita wao, wazimie kwa kustuka!
37
Panga na ziwajie farasi wao na magari yao nao warugaruga walio katikati yao, wawe kama wanawake! Panga na zivijie navyo vilimbiko vyao, vipokonywe!
38
Jua kali na liyapige maji yao, yakauke! Kwani nchi hii ni ya vinyago, nao wenyeji wameingiwa na wazimu kwa ajili ya mifano yao.
39
Kwa hiyo watakaa humo nyama wa porini na mbwa wa mwitu, nao mbuni watakaa mwake, lakini watu hawatakaa humo kale na kale, ila utakaa pasipo mtu kwa vizazi na vizazi.
40
Ndivyo, asemavyo Bwana: Kama Mungu alivyoangamiza Sodomu na Gomora pamoja na vijiji vyao, hivyo napo hapa hapatakaa mtu, wala hapatalala mgeni wa kimtu.
41
Utaona, watu wakija toka kaskazini, tena taifa kubwa na wafalme wengi watainuka mapeoni kwa nchi.
42
Wanashika pindi na mikuki, ni wakorofi, hawana huruma, sauti zao huvuma kama bahari, hupanda farasi, wako tayari kupiga kama mtu wa vitani; wanakujia wewe, binti Babeli.
43
Mfalme wa Babeli amezisikia habari zao; ndipo, mikono yake ilipolegea, masongano yakamshika na uchungu, kama mwanamke anayetaka kuzaa.
44
Kama simba anavyopanda akitoka machakani kwenye Yordani, ajie maboma yenye nguvu, ndivyo, nitakavyowakimbiza kwao kwa mara moja, naye aliyechaguliwa nitamweka kuwa mkuu wao, kwani yuko nani afananaye na mimi? Au yuko nani atakayeniwekea siku? Yuko mchungaji gani atakayesimama usoni pangu?
45
Kwa hiyo lisikieni shauri la Bwana, aliloukatia Babeli, nayo mawazo yake, aliyoiwazia nchi ya Wakasidi kwamba: kweli watakaowakokotakokota ndio wadogo wa makundi, kweli nchi yao yenyewe itawastukia.
46
Kwa mtutumo wa kutekwa kwa Babeli nchi itatetemeka, navyo vilio vitasikilika kwa mataifa.
← Chapter 49
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 51 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52