bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 2
Jeremiah 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 3 →
1
Neno la Bwana likanijia kwamba:
2
Nenda kutangaza masikioni mwao Wayerusalemu kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nayakukumbukia magawio ya ujana wako na upendo wa uchumba wako, uliponifuata nyikani katika nchi isiyowezekana kupandwa mbegu.
3
Hapo Waisiraeli walikuwa wamejitakasa kuwa wa Bwana, wakawa malimbuko ya mavuno yake; wote waliotaka kuwala wakakora manza, mabaya yakawajia; ndivyo, asemavyo Bwana.
4
Lisikilizeni Neno la Bwana ninyi wa mlango wa Yakobo nanyi vizazi vyote vya mlango wa Isiraeli!
5
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Baba zenu waliona mapotovu gani kwangu wakiniacha mbali wakaja kuyafuata yasiyo maana na kufanya wenyewe yasiyo maana?
6
Hawakuuliza: Bwana yuko wapi aliyetutoa katika nchi ya Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi zenye jangwa na makorongo, katika nchi kavu ziuazo, katika nchi zisizopitwa na mtu, zisizokaa mtu?
7
Nilipowapeleka katika nchi ichipukayo vizuri, myale matunda yake na mema yake, basi, hapo mlipoiingia mliitia nchi yangu machafu, iliyokuwa fungu langu mkaigeuza kuwa tapisho.
8
Watambikaji hawakuuliza: Bwana yuko wapi? Wala wenye kazi za Maonyo hawakunijua, wabaya wakanikosea, wafumbuaji wakafumbua mambo ya Baali, wakayafuata yasiyofaa.
9
Kwa hiyo Bwana asema: Kweli inanipasa kufuliza kuwagombeza ninyi, nao wana wa wana wenu nitawagombeza.
10
Haya! Vukeni, mfike pwani kwa Wakiti, mwone! Tumeni watu, waje Kedari, mtambue vema na kuona, kama yamekuwako mambo kama hayo!
11
Mwone, kama liko taifa lililoiacha miungu ya kwao na kufuata mingine, nayo siyo miungu! Nao walio ukoo wangu wameuacha utukufu wao wakifuata yasiyofaa.
12
Yastukeni, ninyi mbingu, mambo kama hayo! Zizimukeni kwa kushangaa kabisa! ndivyo, asemavyo Bwana.
13
Kwani walio ukoo wangu wamefanya mabaya mawili: wameniacha mimi niliye kisima chenye maji ya uzima, kisha wakajichimbia visima vingine, navyo ni visima vyenye nyufa visivyoweza kushika maji.
14
Je? Isiraeli ni mtumwa au mzalia wa nyumbani? Mbona wamekuwa mateka?
15
Simba wanamngurumia na kupaza sauti zao, wakaigeuza nchi yake kuwa mapori tu, miji yake imeteketezwa, haina mwenye kukaa humo.
16
Kisha Wamisri wa Nofu na wa Tahapanesi wakaulisha utosi wako.
17
Kulikokupatia hayo siko kumwacha Bwana Mungu wako, alipotaka kukuongoza njiani?
18
Na sasa kwa sababu gani unakwenda Misri kunywa maji ya Sihori? Tena kwa sababu gani unakwenda Asuri kunywa maji ya lile jito kubwa?
19
Ubaya wako ndio unaokupiga, ubishi wako ndio unaokupatiliza. Yajue, yatazame, ya kuwa kumwacha Bwana Mungu wako ndiko kubaya kwenye uchungu! Nawe hukumwogopa kamwe. Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu wako Mwenye vikosi.
20
Kwani tangu kale ulivivunja vyuma vyako, ukazikata kamba zako, ukasema: Sitaki kumtumikia, ila kila kilima kirefu ulikipanda, hata kivulini kwa kila mti wenye majani mengi ukajilaza chini ukifuata ugoni.
21
Nami ndimi, niliyekupanda, ulipokuwa tawi zuri lenyewe la mzabibu uliozaa matunda yaliyo mazuri kweli; sasa inakuwaje, ukinigeukia na kuleta machipukizi ya mzabibu mgeni?
22
Ijapo ujioshe kwa magadi na kutumia hata sabuni nyingi, uchafu wa ubaya ulioufanya hautoki machoni pangu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
23
Unasemaje? Sikujichafua, sikuyafuata mambo ya Baali? Itazame njia yako ya kwenda bondeni! Yajue, uliyoyafanya huko kwa kuwa kama jike la ngamia ajiendeaye huko na huko kwa nyege zake.
24
Ukawa kama kihongwe cha kike azoeaye nyika, naye hutwetea upepo kwa kukimbizwa na tamaa ya roho yake; tena yuko nani awezaye kuzituliza nyege zake? Lakini amtafutaye hajichokeshi: mwezi wake unapotimia, humwona upesi.
25
Iangalie miguu yako, usivichakaze viatu! Liangalie nalo koo lako, lisipatwe na kiu! Lakini wewe hujibu: Ni kazi bure kunionya, sionyeki, kwani ninapenda wageni, nitawafuata.
26
Kama mwizi anavyoona soni akikamatwa, vivyo hivyo nao wa mlango wa Isiraeli sharti waone soni, wafalme wao na wakuu wao na watambikaji wao na wafumbuaji wao.
27
Maana huuambia mti: Wewe ndiwe baba yangu. Hata jiwe huliambia: Wewe ulinizaa. Lakini mimi wamenigeukia migongo, sizo nyuso; lakini siku za kupatwa na mabaya huniambia: Inuka, utuokoe!
28
Basi, miungu yako, uliyojifanyizia, iko wapi? Na iinuke, kama inaweza kukuokoa, unapopatwa na mabaya! Kama miji yako ilivyo mingi, ndivyo, nayo miungu yako, wewe Yuda, ilivyo mingi.
29
Mbona unanigombeza? Ninyi nyote mmenitengua; ndivyo, asemavyo Bwana.
30
Imekuwa ya bure, nikiwapiga wana wenu, maana hawakuonyeka, panga zenu zikawala wafumbuaji wenu, kama simba wanavyoangamiza.
31
Ninyi mlio uzao mbaya, liangalieni Neno la Bwana! Je? Nimegeuka kuwawia Waisiraeli kama nyika au kama nchi yenye giza? Kwa sababu gani walio ukoo wangu husema: Tumekwisha kujiendea, haturudi kwako tena.
32
Je? Yuko mwanamwali asahauye kujipamba au mchumba asahauye kuvaa yapasayo ndoa? Nao walio ukoo wangu wamenisahau siku zisizohesabika.
33
Unajuaje kuitengeneza njia yako vizuri ukitafuta wapenzi? Kweli hivyo ndivyo, ulivyojifundisha mabaya nayo katika njia zako.
34
Kumbe hata mapindo ya nguo zako yameshikwa na damu zao wakiwa waliouawa pasipo makosa yao yo yote. Nao hukuwapata, wakipokonya, ila ni mambo yayo hayo.
35
Kisha ukasema: Sikukosa kamwe: Kwa hiyo makali yake yameondoka kwangu. Na unione, nikikupatiliza kwa kusema kwako: Sikukosa!
36
Mbona unatangatanga sana, uigeuze njia yako? Hata Wamisri watakutia soni, kama Waasuri walivyokutia soni.
37
Huko nako utatoka, mikono yako ikiwa kichwani, kwani Bwana amewakataa, uliowakimbilia; kwa hiyo hakuna, utakachokipata kwao.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52