bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 7
Jeremiah 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 8 →
1
*Neno lililomjia Yeremia likitoka kwa Bwana ni hili:
2
Simama langoni mwa Nyumba ya Bwana, ulitangaze neno hili huko ukisema: Lisikieni neno la Bwana, ninyi Wayuda wote mnaoingia humu malangoni kumwangukia Bwana!
3
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli: Ziangalieni njia zenu na matendo yenu, yawe mema! Ndipo, nitakapowakalisha katika nchi hii.
4
Msijiegemeze maneno ya uwongo kwamba: Nyumba ya Bwana, Nyumba ya Bwana, Nyumba ya Bwana ni hii!
5
Ila jikazeni, njia zenu na matendo yenu yawe mema, mfanyiziane yanyokayo kila mtu na mwenziwe!
6
Msiwakorofishe wageni wala wafiwao na wazazi wala wajane! Wala msimwage mahali hapa damu zao wasiokosa! Wala msifuate miungu mingine! Maana hivyo mnajipatia mabaya.
7
Ndipo, nitakapowakalisha mahali hapa katika nchi hii, niliyowapa baba zenu, iwe yao tangu kale hata kale.
8
Tazameni! Ninyi mnaojiegemeza maneno ya uwongo yasiyofaa:
9
Huiba, huua, huzini, huapa kwa uwongo, humvukizia Baali, hufuata miungu mingine, msiyoijua.
10
Kisha mnakuja kusimama machoni pangu katika Nyumba hii iliyoitwa kwa Jina langu, mkasema: Tumepona! mpate kuyafanya matapisho hayo yote.
11
Je? Nyumba hii iliyoitwa kwa Jina langu imegeuka kuwa pango la wanyang'anyi machoni penu? Mimi nami ninayaona kweli. Ndivyo, asemavyo Bwana.*
12
Haya! Nendeni mahali pangu kule Silo, nilipolikalisha Jina langu kwanza, myaone yote, niliyopafanyizia kwa ajili ya ubaya wao Waisiraeli walio ukoo wangu!
13
Sasa ndivyo, asemavyo Bwana: nanyi mmeyafanya hayo matendo yote, tena nalisema nanyi pasipo kuchoka kusema, lakini hamkusikia, nikawaita, lakini hamkuitikia.
14
Kwa hiyo nitaifanyizia Nyumba hii iliyoitwa kwa Jina langu, ninyi mnayoitumia ya kujiegemezea, hata mahali hapo, nilipowapa ninyi na baba zenu, nitapafanyizia, kama nilivyofanya huko Silo.
15
Nitawatupa, mwondoke machoni pangu, kama nilivyowatupa ndugu zenu wote pia walio kizazi chake Efuraimu.
16
Wewe nawe usiwaombee wao wa ukoo huu! Wala usipaze sauti kunilalamikia kwa ajili yao, wala usinihimize! Kwani hapo sikusikii.
17
Huyaoni, wanayoyafanya katika miji ya Yuda namo Yerusalemu katika barabara zake?
18
Watoto huokota kuni, nao baba huziwasha moto, wanawake wakikanda unga wa kufanya vikate vya mfalme wa kike wa mbinguni, tena humwaga vinywaji vya kutambikia miungu mingine, kusudi waniumize moyoni.
19
Ndivyo, asemavyo Bwana: Hao watakao kuniumiza mimi hawajiumizi wenyewe, nyuso zao zipate kutiwa soni?
20
Kwa hiyo hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wataona, jinsi makali yangu yenye moto yatakavyomwagwa mahali hapa, yachome watu na nyama na miti ya mashamba na mazao ya nchi, yawake moto usiozimika.
21
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Ng'ombe zenu za tambiko za kuteketezwa nzima ziongezeni kwa ng'ombe zenu za tambiko za kuchinjwa, mpate kula nyama.
22
Kwani sikuwaambia baba zenu, wala sikuwaagiza, nilipowatoa katika nchi ya Misri, watoe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za kuchinjwa.
23
Kweli niliwaagiza neno hili tu kwamba: Isikieni sauti yangu! Ndivyo, nitakavyokuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa ukoo wangu. Kisha zishikeni njia zote, nitakazowaagiza, mpate kuona mema!
24
Lakini hawakusikia, wala hawakuyatega masikio yao, wakaendelea kwa mashauri na kwa ushupavu wa mioyo yao mibaya, wakanionyesha migongo, lakini sizo nyuso.
25
Vikawa hivyo tangu siku ile, baba zenu walipotoka katika nchi ya Misri mpaka siku hii ya leo; nami nalituma kwenu watumishi wangu wote walio wafumbuaji, sikuchoka hata siku moja.
26
Lakini hawakunisikia, wala hawakuyatega masikio yao, wakazishupaza kosi zao, wakafanya mabaya kuwashinda baba zao.
27
Nawe ukiwaambia maneno haya yote, hawatakusikia, ukiwaita, hawatakuitikia.
28
Basi, uwaambie: Taifa hili ndilo lisiloisikia sauti ya Bwana Mungu wao, wala hawakutaka kuonyeka. Welekevu umepotea, umetoweka vinywani mwao.
29
Binti Sioni, zinyoe nywele zako za urembo, uzitupe! Piga kilio vilimani juu kusikokuwa na vijiti! Kwani Bwana amekikataa kizazi kilichomkasirisha, akakitupa.
30
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Wana wa Yuda wamefanya yaliyo mabaya machoni pangu, wakaweka matapisho yao katika Nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, waichafue.
31
Wakapajenga pa kumtambikia Tofeti katika bonde la Mwana wa Hinomu, wateketeze hapo motoni wana wao wa kiume na wa kike; nami sikuwaagiza hivyo, wala havikunijia moyoni.
32
Kwa hiyo ndivyo, asemavyo Bwana: Wataona kweli, siku zikija, pasipotajwa tena Tofeti wala bonde la Mwana wa Hinomu, ila pataitwa Bonde la Uuaji; ndipo, watakapozikia kwenye Tofeti kwa kukosa pengine.
33
Nayo mizoga ya watu wa ukoo huu itakuwa chakula cha ndege wa angani na cha nyama wa porini, asiweko atakayewatisha.
34
Ndipo, nitakapokomesha katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu sauti za vicheko na sauti za furaha, hata sauti za wachumba wa kiume na wa kike, kwani nchi hii itakuwa mavunjiko tu.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52