bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 1
Isaiah 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 2 →
1
Haya ndiyo maono ya Yesaya, mwana wa Amosi, aliyoyaona kwa ajili ya Yuda na kwa ajili ya Yerusalemu siku za Uzia na za Yotamu na za Ahazi na za Hizikia, waliokuwa wafalme wa Yuda.
2
Sikilizeni, ninyi mbingu! Angalieni, ninyi nchi! Kwani Bwana anasema: Nilikuza wana, nikawapa utukufu; lakini wao wamenitengua.
3
Ng'ombe humjua bwana wake. naye punda hupajua, mabwana wake wanapomwekea chakula; lakini Isiraeli hanijui, walio ukoo wangu hawanitambui.
4
Utaona, wewe kabila lenye makosa, nanyi mnaolemewa na manza, mlizozikora, wewe kizazi cha wabaya, nanyi wana wapotovu! Wamemwacha Bwana na kumbeza Mtakatifu wa Isiraeli, wakarudi nyuma.
5
Mnapigiwa nini, kwa kuwa mnafuliza bado kurudi nyuma? Kila kichwa kiko na vidonda, kila moyo umeugua.
6
Toka wayo wa mguu mpaka kichwani hapana palipo pazima, ni madonda na machubuko na mapigo matupu; hayaoshwi, wala hayakufungwa, wala hayakulegezwa na mafuta.
7
Nchi yenu ni mapori tu, miji yenu imeteketezwa na moto, mashamba yenu yanaliwa na wageni machoni penu; kweli ni mapori tu, kama nchi zilivyo zikiharibiwa na wageni.
8
Paliposalia ni penye binti Sioni, ni kama kilindo mizabibuni, ni kama dungu shambani kwa miboga, kweli ni kama mji uliozungukwa na adui.
9
Bwana Mwenye vikosi kama asingalitusazia hao wachache waliookoka, tungalikuwa kama Sodomu, tungalifanana na Gomora.
10
Lisikilizeni neno lake Bwana, ninyi waamuzi wa Sodomu! Yaangalieni maonyo yake Mungu wetu, ninyi watu wa Gomora! Bwana anasema: Ni vya nini
11
vipaji vyenu vingi, mnavyonitolea vya tambiko? Nimeshiba kondoo, mlionichomea, hata mafuta ya ndama wanonao, damu zao ng'ombe na wana kondoo na mbuzi hazinipendezi.
12
Mnapokuja kuoneka machoni pangu, ni nani aliyevitaka hivyo mikononi mwenu, mkija kuzikanyaga nyua zangu?
13
Acheni kuleta tena vilaji vya tambiko visivyofaa! Uvumba nao hunitapisha, hata sikukuu za miandamo ya mwezi nazo za mapumziko na za makusanyiko; sivumilii, upotovu ukiwa hapohapo, mnaponikusanyikia.
14
Roho yangu huzichukia sikukuu zenu za miandamo ya mwezi nazo sikukuu zenu nyingine, zimeniwia mzigo mzito, nimechoka kuuchukua tena.
15
Mkininyoshea mikono yenu, nitayafumba macho yangu, yasiione, hata mkikaza kuniomba, sisikii; maana mikono yenu imejaa damu.
16
Iosheni na kuitakasa! Uondoeni ubaya wa matendo yenu, macho yangu yasiuone tena! Msiendelee na kufanya mabaya!
17
Jifundisheni kufanya mema! Tafuteni njia ya kunyosha maamuzi mkiwapingia wakorofi! Waamulieni wafiwao na wazazi! Wagombeeni wajane!
18
Njoni, tuumbuane! Ndivyo, asemavyo Bwana. Makosa yenu ijapo yawe mekundu kama damu, yatakuwa meupe kama chokaa juani; ijapo yawe mekundu kama nguo za kifalme, yatakuwa kama pamba.
19
Ikiwapendeza, mnisikie, basi, mtakula mema ya nchi.
20
lakini mkikataa, mkaacha kutii, mtaliwa na panga. Kwani kinywa chake Bwana kimesema.
21
Kumbe mji uliokuwa wenye welekevu umegeuka kuwa wenye ugoni! Ulikuwa umejaa maamuzi yanyokayo, wongofu ukapata kao kwako, lakini sasa ni kao la wauaji.
22
Fedha yako imegeuka kuwa mavi ya chuma tu, mvinyo yako imechanganywa na maji.
23
Wakuu wako hufanya fujo, wenzao ni wezi, wao wote hupenda matunzo, hufuata fedha za kupenyezewa, wafiwao na wazazi hawawaamulii, wala mashauri ya wajane hayafiki kwao.
24
Kwa sababu hiyo ndivyo, asemavyo Bwana, yeye Bwana Mwenye vikosi amtawalaye Isiraeli: Patafika, nitakapojituliza kwao wapingani wangu, nikiwalipiza adui zangu!
25
Ndipo, mkono wangu utakapokurudia tena, hapo nitayayeyusha mavi yako ya chuma kwa dawa kali, niyaondoe yasiyokupasa yote yaliyomo.
26
Kisha nitakupa tena waamuzi kama huko kale, nao wakata mashauri watakuwa kama wao wa mwanzoni. Kwa hiyo utaitwa Ngome ya Wongofu au Mji wenye Welekevu.
27
Sioni utakombolewa kwa maamuzi ya kweli, nao watu wake walioigeuza mioyo watakombolewa kwa wongofu.
28
Lakini wapotovu na wakosaji watavunjwa wote pamoja, nao waliomwacha Bwana watatoweka.
29
Kwani watatwezwa kwa ajili ya mitamba, mliyoitunukia, nazo nyuso zenu zitaiva kwa kuona soni kwa ajili ya mashamba, mliyoyachagua.
30
Kwani mtakuwa kama mtamba uliokauka pamoja na majani yake, au mtafanana na shamba lisilo na maji.
31
Mwenye nguvu atageuka kuwa kama madifu makavu, nazo kazi zake zitakuwa kama cheche la moto; kisha yatateketea yote pamoja, asipatikane awezaye kuuzima moto huo.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66