bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 22
Isaiah 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 23 →
1
Mmeona nini mkipanda wote vipaani?
2
Wewe mji uliojaa makelele ya machafuko, mliomo na wapiga vigelegele, watu wako waliouawa hawakuuawa kwa panga, wala hawakufa vitani.
3
Wakuu wako wamekimbia wote pamoja, wakatekwa pasipo upindi, nao watu wako waliopatikana wametekwa wote, nao waliokimbia mbali.
4
Kwa hiyo nimesema: Msinitumbulie macho, nilie kwa uchungu! Wala msinibembeleze na kunituliza moyo kwa ajili ya kuangamia kwao walio wazaliwa wa ukoo wangu!
5
Kwani siku ya mastuko na ya maangamizo na ya machafuko imetoka kwake Bwana Mungu Mwenye vikosi, ikaja Bondeni kwenye Maono, ni siku iliyobomoa maboma, vilio vyake vikasikilika mlimani.
6
Waelamu wameshika mapodo, wakapanda magari na farasi, Wakiri nao wakazifunua ngao.
7
Ndipo, mabonde yako mazuri yalipojaa magari, nao wapanda farasi wakajisimamisha upande wa lango la maji.
8
Hivyo akayafunua, ambayo Wayuda walijifunika nayo, siku ile wakayatazamia mata yaliyowekwa katika nyumba ya mwituni.
9
Mkapaona, mji wa Dawidi ulipobomokabomoka, ya kuwa ni pengi, mkayakusanya maji ya ziwa la chini.
10
Mkazihesabu nazo nyumba za Yerusalemu, mkabomoa nyingine, mpate ya kuujengajenga ukuta wa boma.
11
Katikati ya kuta mbili za boma mkatengeneza mahali, pawe pa kukusanyia maji ya ziwa la kale. Lakini yeye aliyeyafanya mambo hayo hamkumtazama, hamkumwona aliyeyalinganya, yalipokuwa yangaliko mbali.
12
Bwana aliye Bwana Mwenye vikosi aliwaita siku ile, mlie na kuomboleza, mnyoe vichwa na kuvaa magunia.
13
Kumbe mkacheza na kufurahi, mkaua ng'ombe, mkachinja nao kondoo, mkala nyama, mkanywa mvinyo, mkasema: Na tule, na tunywe! Kwani kesho tutakufa!
14
Kwa hiyo Bwana Mwenye vikosi ameyafumbua masikioni mwangu: Mpaka mtakapokufa, hamtaondolewa kabisa manza hizi, mlizozikora. Ndivyo, anavyosema Bwana Mungu Mwenye vikosi.
15
Ndivyo, anavyosema Bwana Mungu Mwenye vikosi: Nenda, uje kwake huyo mtunza mali, huyo Sebuna aliye mkuu wa nyumba ya mfalme.
16
Unafanya nini hapa? Kuna nani wa kwenu huku? Kumbe unajichimbia kaburi hapa! Kweli unajichimbia hapa juu kaburi lako, unajichongea magengeni kao lako!
17
Tazama, Bwana atakutupa na kukubwaga kwa nguvu! Wewe mtu wa kiume atakukunja kabisa.
18
Atakuzinga, uviringane kama mpira, akutupe katika nchi iliyopanuka pande mbili; ndiko, utakakokufa, ndiko, magari yako mazuri yatakakokufuata wewe uliyeitweza Nyumba ya Bwana wako.
19
Nitakutangua katika utunzaji wako, nitakuondoa katika usimamizi wako.
20
Siku ile ndipo, nitakapomwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia.
21
Nitamvika kanzu yako, nitamfunga nao mshipi wako, utunzaji wako nitampa, uwe mkononi mwake, atakuwa baba yao wakaao Yerusalemu, hata baba yao walio wa mlango wa Yuda.
22
Nitampa ufunguo wa nyumba ya Dawidi, uwe begani pake; atakapofungua, hatakuwako awezaye kupafunga, atakapofunga, hatakuwako awezaye kupafungua.
23
Nitampigilia kama msumari mahali pagumu, atauwia lango wa baba yake kiti chenye utukufu.
24
Kwake utatundikwa utukufu wote wa mlango wa baba yake; miche na machipukizi na vyombo vyote vidogo, kuanzia vikombekombe kufikisha mitungitungi yote.
25
Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Msumari uliokuwa umepigiliwa mahali pagumu siku ile uvunjike, utajipinda, uanguke chini, nao mzigo ulioangikwa kwake utaanguka, kwani Bwana amevisema.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66