bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 44
Isaiah 44
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 45 →
1
*Sasa sikia mtumishi wangu Yakobo! Nawe Isiraeli, niliyemchagua!
2
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana aliyekuumba, aliyekutengeneza tumboni mwa mama, anayekusaidia: Usiogope, mtumishi wangu Yakobo, nawe Isiraeli uongokaye, niliyemchagua!
3
Kwani nitamwaga maji panapo kiu, nitokeze mito pakavu, nitaimwaga Roho yangu kwao walio uzao wako, nayo mbaraka yangu kwao walio miche yako.
4
Watakuwa kama majani kwenye maji au kama mifuu kwenye mito yenye maji.
5
Huyu atasema: Mimi ni wake Bwana, naye mwenziwe atajiita kwa jina la Yakobo, naye mwingine ataandika mikononi mwake: Wa Bwana, mwingine atajivunia jina la Isiraeli,
6
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana, mfalme wa Isiraeli, aliye mkombozi wake, yeye Bwana Mwenye vikosi: Mimi ni wa mwanzo na wa mwisho, pasipo mimi hakuna Mungu.*
7
Yuko nani anayefanana na mimi? Na apaze sauti, ayatangaze! Tena anieleze, kama ni kwa sababu gani, nikiweka ukoo wa watu kuwa wa kale na kale. Hata yajayo nayo yatakayokuja na wayatangazie watu!
8
Msistuke, wala msitetemeke! Kumbe sikukuambia hayo toka kale na kuyatangaza? Ninyi m mashahidi wangu: Yuko Mungu pasipo mimi? Hakuna mwamba mwingine, nisioujua.
9
Watengenezao vinyago wote si kitu, navyo viumbe vyao vya kupendeza havifai, wanaovishuhudia wenyewe hawaoni, wala hawatambui kazi, ambazo vilizifanya, kusudi wapatwe na soni.
10
Ni nani aliyetengeneza mungu na kuyeyusha kinyago kisichofaa kitu?
11
Tazameni! Wote walio upande wao hupatwa na soni, nao mafundi na watu tu. Na wakusanyike wote pamoja na kusimama hapa, wote pamoja watastuka na kupatwa na soni.
12
Mhunzi huvishika vyombo vyake, hutumia moto wa makaa akivitengeneza vinyago kwa vyundo; hivyo anavimaliza kwa mkono wake wenye nguvu; lakini asipokula, nguvu hupotea, napo asipokunywa hulegea.
13
Fundi wa kuchonga miti huipima kwa kamba na kuiandika kwa kalamu; kisha hutumia visu na kupimapima tena penye kuviringana. Hivyo anatengeneza kinyago, kifanane na mtu mwenye utukufu wa kimtu, kikae nyumbani.
14
Huagiza watu, wamkatie miangati, huchukua hata mipingo na mivule, hujichagulia miti ya mwituni iliyo migumu, hupanda nayo mise, mvua iikuze.
15
Watu huitumia ya kuchoma moto, huchukua vibanzi vyao vya kuotea, vingine huvitumia jikoni vya kuchomea mikate, tena kipande hukitengeneza kuwa mungu wa kuuangukia; alipokwisha kufanya kinyago, hukitambikia.
16
Hivyo hutumia kipande cha mti cha kuchoma moto, apate kuota, kipande cha kupikia nyama, ale nazo zilizochomwa, ashibe, apate hata jasho, aseme: A, nimepata jasho, nimeona moto!
17
Kipande kinachosalia hukitengeneza kinyago kuwa mungu, hukitambikia na kukiangukia na kukilalamikia kwamba: Niponye! Kwani mungu wangu ndiwe wewe!
18
Lakini hawa hawavijui wala hawavitambui, kwani macho yao yamegandamana, yasione, mioyo yao isielewe maana.
19
Hakuna ayawazaye moyoni, wala hakuna ayajuaye na kuyatambua kwamba: Kipande chake nimekichoma moto, kipande nimetumia makaa yake, yachome mkate, kipande nimechoma cha kuchomea nyama, nikala. Tena sao lake nilitengeneze kuwa chukizo, nitambikie kilicho kipande cha mti?
20
Ni hivyo: Achungaye majivu moyo wake umedanganyika, ukampoteza, asiiponye roho yake, wala asiseme: Siyo yenye uwongo yaliyomo mkononi mwangu?
21
Haya yakumbukeni, Yakobo na Isiraeli! Kwani wewe ndiwe mtumishi wangu; nimekutengeneza wewe kuwa mtumishi wangu, wewe Isiraeli hutasahauliwa kwangu.
22
Nimeyatowesha mapotovu yako kama wingu, nayo makosa yako kama kungugu. Rudi kwangu! Kwani nimekukomboa.
23
Shangilieni, mbingu, ya kuwa Bwana ameyatimiza! Pigeni kelele, vilindi vya kuzimuni! Pigeni shangwe na kupaza sauti, milima na misitu na miti yote iliyomo! Kwani Bwana amemwokoa Yakobo, nako kwake Isiraeli anautokeza utukufu wake.
24
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana, mkombozi wako, aliyekutengeneza tumboni mwa mama: Mimi Bwana niliyafanya yote. Mimi nilipoziwamba mbingu peke yangu, nikazitanda hata nchi, yuko nani aliyekuwa kwangu?
25
Ndege, wapuzi wanazoziona, nazibezesha, nao waaguaji nawalevya, nao walio werevu wa kweli nawarudisha nyuma, ujuzi wao naugeuza kuwa ujinga.
26
Neno la mtumishi wake hulisimamisha, nayo mashauri ya wajumbe wake huyatimiza. Ni yeye auambiaye Yerusalemu: Na ukaliwe! Nayo miji ya Yuda anaiambia: Jengweni! Nami nitayasimamisha mabomoko yao!
27
Kilindi cha maji anakiambia: Kauka! mimi nitaipwelesha mito yako.
28
Yeye ndiye anayemwambia Kiro: Huyu ndiye mchungaji wangu atakayeyatimiza mapenzi yangu yote. Hivyo Yerusalemu utajengwa, nalo Jumba takatifu litawekewa misingi.
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 45 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66