bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 43
Isaiah 43
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 42
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 44 →
1
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana aliyekuumba, Yakobo, aliyekutengeneza, Isiraeli: Sasa usiogope! Kwani nimekukomboa, nimekuita kwa jina lako, ndiwe wangu!
2
Utakapopita majini, mimi niko pamoja na wewe; utakapopita katika majito, hayatakutosa; utakapopita motoni hutachomwa, wala ndimi za moto hazitakuunguza.
3
Kwani mimi Bwana Mungu wako, Mtakatifu wa Isiraeli, mimi mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa makombozi yako, nikatoa Nubi na Seba mahali pako.
4
Kwa kuwa uliwaziwa machoni pangu kuwa mali, umepata utukufu, nikakupenda. Kwa hiyo nimetoa watu, nikukomboe, hata makabila mazima, niikomboe roho yako.
5
Usiogope! Kwani mimi niko pamoja na wewe; walio uzao wako nitawaleta na kuwatoa maawioni kwa jua, nitawakusanya na kuwatoa nako machweoni kwa jua.
6
Nitauambia upepo wa kaskazini: Watoe! nao upepo wa kusini: Usiwazuie! Walete wanangu wa kiume na kuwatoa mbali nao wanangu wa kike na kuwatoa mapeoni kwa nchi,
7
wao wote waitwao kwa Jina langu! Ndio, niliowaumba, nijipatie utukufu, ndio, niliowatengeneza na kuwafanya.
8
Watokezeni watu walio vipofu! Tena macho wanayo. Nao walio viziwi! Tena masikio wanayo.
9
Wamizimu wote na wakusanyike pamoja, makabila ya watu na yakutane; kwao yuko nani aliyetangaza kama hayo? Yuko nani aliyetuambia yale ya mbele? Na watoe mashahidi, wapate kushinda shaurini, watu wayasikie, kisha waseme: Ni kweli!
10
Ninyi m mashahidi wangu! ndivyo, asemavyo Bwana, u mtumishi wangu, niliyekuchagua kwamba: Mjue, mpate kunitegemea, tena mtambue, ya kuwa mimi ndiye! Mbele yangu hakufanyika Mungu, hata nyuma yangu hatakuwa.
11
Mimi ndimi Bwana, pasipo mimi hakuna mwokozi.
12
Mimi nimeyatangaza, nikatengeneza wokovu, nikaujulisha, mkingali hamna mungu mgeni kwenu; nanyi m mashahidi wangu, nami ndimi Mungu! ndivyo, asemavyo Bwana.
13
Tena tangu leo nitakuwa yeye niliyekuwa, hakuna aopoaye mkononi mwangu; nikitaka kufanya kitu, yuko nani atakayekizuia?
14
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana, mkombozi wenu, aliye Mtakatifu wa Isiraeli: Kwa ajili yenu nilituma watu kwenda Babeli, niwakimbize wote pia, washuke mtoni, nao Wakasidi na wakimbie katika vyombo vyao, walivyovipigia shangwe.
15
Mimi Bwana ndimi Mtakatifu wenu, mimi niliyemwumba Isiraeli ndimi mfalme wenu.
16
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana awekaye njia baharini, hata mapito katika maji yenye nguvu,
17
atokezaye magari na farasi, vikosi na wakuu pamoja: Mara wataanguka, wasiinuke tena, watazimia, kama utambi unavyozimika.
18
Msiyakumbuke yaliyoko mbele, wala msiyatambue yaliyopita kale!
19
Tazameni! Ninafanya mapya, nayo yameanza kuchipuka! Nanyi hamjayaona bado? Hata nyikani ninatoa njia, nako jangwani majito.
20
Nyama wa porini watanitukuza, mbwa wa mwitu na mbuni, kwa kuwa nimetoa maji nyikani na majito jangwani, niwanyweshe wao, niliowachagua, wawe ukoo wangu.
21
Hao watu, niliojitengenezea, watayasimulia na kushangilia.
22
Nawe Yakobo, hukuniita mimi, nawe Isiraeli, hukujichokesha kwa ajili yangu.
23
Hukuniletea wana kondoo wako kuwa wa kunitambikia, wala hukuniheshimu na kunitolea vipaji vya tambiko. Nami sikukusumbua, unipatie matunzo, wala sikukuchokesha na kutaka uvumba kwako.
24
Hukuninunulia vipande vya kichiri na kutoa fedha zako, wala hukuninywesha mafuta ya ng'ombe zako za tambiko. Ila ulinisumbua kwa makosa yako, ukanichokesha kwa manza zako, ulizozikora.
25
Mimi ninayafuta mapotovu yako kwa ajili yangu mimi, nayo makosa yako sitayakumbuka tena.
26
Nikumbushe, tubishane! Nawe yaseme yako, upate kushinda humu shaurini!
27
Baba yako wa kwanza alikosa naye, nao wasemaji wako walinitengua.
28
Ndipo, nilipowatia mwiko wakuu wa Patakatifu, nikamtoa Yakobo kuwa wa kuapizwa naye Isiraeli kuwa wa kufyozwa.
← Chapter 42
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 44 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66