bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 36
Isaiah 36
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 37 →
1
Ikawa katika mwaka wa 14 wa mfalme Hizikia, ndipo, Saniheribu, mfalme wa Asuri, alipoipandia miji yote ya Wayuda iliyokuwa na maboma, akaiteka.
2
Kisha mfalme wa Asuri akamtuma mkuu wa askari, atoke Lakisi kwenda Yerusalemu na kikosi kikubwa kwake mfalme Hizikia. Akaja kusimama kwenye mfereji wa ziwa la juu katika barabara iendayo Shambani kwa Dobi.
3
Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa mtunza nyumba ya mfalme, na Sebuna aliyekuwa mwandishi na Yoa, mwana wa Asafu, aliyekuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa wakamtokea.
4
Mkuu wa askari akawaambia: Mwambieni Hizikia: Hivi ndivyo, mfalme mkuu, mfalme wa Asuri, anavyosema: Hilo egemeo, unaloliegemea, ndio nini?
5
Nasema: Ni maneno ya midomo tu, ukisema: Nimekata shauri na kujipa moyo wa kupiga vita. Sasa unamwegemea nani, ukinikataa na kuacha kunitii?
6
Tazama! Egemeo lako, unaloliegemea, ni Misri, hilo fimbo la utete unyongekao! Mtu akilikongojea, litamwingia kiganjani, limchome. Ndivyo, Farao, mfalme wa Misri, anavyowawia wote waliomwegemea.
7
Ukiniambia: Tunamwegemea Bwana Mungu wetu, basi, yeye siye, ambaye Hizikia aliwakataza watu kumtambikia vilimani pake napo penye meza zake za kutambikia, alipowaambia Wayuda na Wayerusalemu: Sharti mmwangukie mbele ya meza hii tu ya kumtambikia?
8
Sasa na upinge na bwana wangu, mfalme wa Asuri: Nitakupa farasi 2000, kama wewe unaweza kujipatia watu wa kuwapanda.
9
Usipowapata utawezaje kuuelekeza nyuma uso wa mwenye amri mmoja tu, ijapo awe mdogo katika watumishi wa bwana wangu? Tena unawaegemea Wamisri, kwa kuwa wako na magari na wapanda farasi.
10
Bwana alikuwa hayuko, nilipoipandia sasa nchi hii, niiangamize? Bwana ndiye aliyeniambia: Ipandie nchi hii, uiangamize!
11
Ndipo, Eliakimu na Sebuna na Yoa walipomwambia mkuu wa askari: Sema Kishami na watumishi wako! Kwani tunakisikia; usiseme na sisi Kiyuda masikioni pa watu hawa walioko ukutani!
12
Mkuu wa askari akawajibu: Je? Bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kwako kuyasema haya maneno? Sio kwa watu hawa wanaokaa ukutani watakaokula pamoja nanyi mavi yao na kunywa mikojo yao?
13
Kisha mkuu wa askari akatokea, akapaza sauti sana na kusema Kiyuda kwamba: Yasikilizeni maneno ya mfalme mkuu, mfalme wa Asuri!
14
Hivi ndivyo, mfalme anavyosema: Hizikia asiwadanganye! Kwani hataweza kuwaponya ninyi.
15
Wala Hizikia asiwaegemeze Bwana kwamba: Bwana ndiye atakayetuponya, mji huu hautatiwa mkononi mwa mfalme wa Asuri.
16
Msimwitikie Hizikia! Kwani hivi ndivyo, mfalme wa Asuri anavyosema: Fanyeni na mimi maagano ya mbaraka, mje kunitokea, mpate kula kila mtu mazao ya mzabibu wake na ya mkuyu wake, mpate kunywa kila mtu maji ya shimo lake mwenyewe,
17
mpaka nitakapokuja, miwachukue kuwapeleka katika nchi iliyo kama nchi yenu. Nayo ni nchi inayojaa ngano na pombe, ni nchi yenye vyakula na mizabibu.
18
Hizikia asiwapoteze na kusema: Bwana atatuponya! Je? Miungu ya wamizimu iliweza mmoja tu kuiponya nchi yake, isichukuliwe na mfalme wa Asuri?
19
Ilikuwa wapi miungu ya Hamati na ya Arpadi? Ilikuwa wapi miungu ya Sefarwaimu? Hata Samaria haikuweza kuiponya, nisiichukue!
20
Katika miungu yote ya nchi hizi ni ipi iliyoweza kuziponya nchi zao, nisizichukue? Basi, Bwana atawezaje kuuponya Yerusalemu, nisiuchukue?
21
Wakanyamaza, hawakumjibu neno, kwani mfalme alikuwa amewaagiza kwamba: Msimjibu!
22
Kisha Eliakimu, mwana wa Hilikia, aliyekuwa mtunza nyumba ya mfalme, na Sebuna aliyekuwa mwandishi na Yoa, mwana wa Asafu, aliyekuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa wakaja kwa Hizikia wenye nguo zilizoraluliwa, wakamsimulia maneno ya mkuu wa askari.
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 37 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66