bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 9
Isaiah 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 10 →
1
Lakini huko kuliko na masongano kama hayo giza haitakaa kabisa. Siku za mbele nchi ya Zebuluni na nchi ya Nafutali alizitia soni, lakini huko nyuma atazipatia utukufu kwenye njia ya baharini na ng'ambo ya Yordani, Galilea ya wamizimu iliko.
2
Watu waliofanya mwendo gizani wameona mwanga mkuu, waliokaa penye kivuli kiuacho mwanga umemulika juu yao.
3
Wewe umekuza watu, wawe wengi, ukawapatia furaha kuu; wanakufurahia, kama watu wanavyofurahi penye mavuno, kama wanavyoshangilia wakigawanya mateka.
4
Kwani umeivunja miti ya kuchukulia mizigo pamoja na magongo yaliyowapiga migongoni, nazo fimbo za wasimamizi, kama ulivyofanya siku ya kuwapatiliza Wamidiani.
5
Kwani mata yote, waliyoyashika kwenye mapigano, nazo nguo zilizofuliwa katika damu zitateketezwa kwa ukali wa moto.
6
*Kwani tumezaliwa mtoto, tumepewa mwana wa kiume, nao ufalme uko begani pake. Jina lake wanamwita: Ajabu la mizungu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa kale na kale, Mfalme wa utengemano.
7
Ufalme wake ni mkubwa, nao utengemano hauna mwisho kwenye kiti cha Dawidi na katika nchi zote, azitawalazo; atazitengeneza na kuzishikiza akiziamua kwa wongofu kuanzia sasa na kuendelea vivyo hivyo kale na kale. Bwana Mwenye vikosi atajihimiza kuyafanya hayo.*
8
Bwana alituma neno la kuwatisha wa Yakobo, linawapasa Waisiraeli nao.
9
Watu wote watalitambua, kama Waefuraimu nao wakaao Samaria wasemao kwa majivuno na kwa mawazo makuu ya mioyo yao kwamba:
10
Majengo ya matofali yalipoanguka, tutapajenga kwa mawe ya kuchonga; mitamba ilipokatwa, tutapanda miangati mahali pao.
11
Kwa hiyo Bwana alipandisha kwao vikosi vya Resini, viwasonge, nao adui zao akawachochea, wawajie:
12
upande wa mbele wakaja Waasuri upande wa nyuma Wafilisti, wakawala Waisiraeli na kuasama vinywa kabisa. Lakini kwa hayo yote makali yake hayajatulia bado, nao mkono wake ungaliko umekunjuka.
13
Nao walio ukoo wake hawakurudi kwake aliyewapiga, Bwana Mwenye vikosi hawakumtafuta.
14
Basi, siku moja Bwana alikata kwao Waisiraeli kichwa na mkia, hata makuti na majani.
15
Kichwa ndio wazee na wenye macheo, mkia ndio wafumbuaji wafundishao mambo ya uwongo.
16
Kwani viongozi wa ukoo huu walikuwa wapotevu, nao walioongozwa nao wakaangamizwa.
17
Kwa sababu hii Bwana hakupendezwa na vijana wao, hakuwahurumia wala waliofiwa na wazazi wala wajane wao, kwani hao wote humbeza Mungu kwa kufanya mabaya, kila kinywa husema mapumbavu. Lakini kwa hayo yote makali yake hayajatulia bado, nao mkono wake ungaliko umekunjuka.
18
Kwani kule kumbeza Mungu kuliendelea kama moto uwakao. unakula miiba na mibigili mikavu, unachoma vichaka vya msituni na kupandisha mawingu mazima ya moshi.
19
Nchi ikateketea kwa moto wa makali ya Bwana Mwenye vikosi, watu wakawa kama chakula cha moto, kwa hiyo hakuwako aliyemwonea ndugu yake uchungu.
20
Wakajikatia kuumeni, lakini njaa haikuondoka; wakala nako kushotoni, lakini hawakushiba; kisha wakala kila mtu nyama ya mkono wake:
21
Manase akamla Efuraimu, naye Efuraimu akamla Manase, kisha wote wawili pamoja wakamgeukia Yuda. Lakini kwa hayo yote makali yake hayajatulia bado, nao mkono wake ungaliko umekunjuka.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66