bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 14
Isaiah 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 15 →
1
Kwani Bwana atawahurumia wa Yakobo, atawachagua Waisiraeli tena, awarudishe katika nchi yao, watue kuko huko, hata wageni wataandamana nao, wajitie katika mlango wa Yakobo.
2
Watu wengine watawachukua, wawapeleke kwao, kisha mlango wa Isiraeli utawatumia katika nchi ya Bwana kuwa watumishi wao wa kiume na wa kike. Hivyo watawateka waliowateka, wawatawale waliowasonga.
3
Hapo Bwana atakapokupatia pa kutulia na kuyapumzikia masumbufu na mahangaiko na matumishi yako magumu, waliyokutumikisha,
4
utamwimbia mfalme wa Babeli wimbo huu wa kumfyoza kwamba: Kumbe mwenye kusonga ametulia! Kumbe napo tulipoumizwa pametulia!
5
Bwana amezivunja fimbo zao wasiomcha, fimbo zao waliotutawala!
6
Ni zile fimbo zao walioyapiga makabila ya watu kwa ukali pasipo kukoma. Ni fimbo zao walioponda mataifa mazima wakiyakanyaga kwa ukali tu pasipo huruma.
7
Nchi yote nzima imetulia kimya, wote pia wanapiga shangwe.
8
Hata mivinje imefurahi pamoja na miangati ya Libanoni kwamba: Tangu hapo ulipotulizwa hakuna aliyepanda kutukata.
9
Kule chini kuzimuni kumevurugika kwa ajili yako: kwa kungoja, uje, kukawaamsha wazimu wote, waliokuwa wenye nguvu katika nchi, kukawainua wafalme wote, wao wa kimizimu, waondoke katika viti vyao vilivyo vya kifalme.
10
Wote pamoja wanakuzomea kwamba: Kumbe nawe umegeuzwa kuwa mnyonge kama sisi! Ukafananishwa kuwa sawasawa kama sisi!
11
Kumbe nao utukufu wako umekumbwa kushuka kuzimuni pamoja na milio ya mapango yako! Chini umetandikiwa funyo kuwa kilalio chako, nalo blanketi lako la kujifunika ni vidudu.
12
Kumbe umeanguka toka mbinguni, ulimokuwa nyota yenye mwanga uliokuwa kama mwanga wa macheche ya jua! Kumbe umepondwa, ukaanguka chini uliyeyalaza mataifa chini yako!
13
Nawe ulijiwazia moyoni mwako kwamba: Na nipande mbinguni kwenye nyota za Mungu, nikisimike kiti changu cha kifalme huko juu, nikae mlimani kwa miungu mapeoni kwa kaskazini!
14
Na nipande kupita mawingu yaliyoko mbinguni juu, nijifananishe kuwa sawasawa naye Mwenyezi!
15
Kumbe umeshushwa kuzimuni mapeoni kwenye mashimo!
16
Wakuonao watakutumbulia macho, wakutambue kwamba: Je? Huyu siye aliyeitetemesha nchi, aliyewatikisa nao wafalme?
17
Je? Siye aliyezigeuza nchi kuwa mapori tu? Je? Siye aliyebomoa miji mizima? Je? Siye aliyewakataza wafungwa wake, wasirudi kwao?
18
Wafalme wote wa kimizimu hulala kwenye utukufu, kila mtu chumbani mwake;
19
lakini wewe umetupwa mbali, usifike kaburini mwako, ukawa kama tawi litapishalo watu, ukafunikwa na mizoga yao waliochomwa kwa panga, waliotupwa mashimoni kwenye majiwe, ukawa kama kibudu kinachokanyagwa.
20
Wewe hutafika kaburini pamoja nao wale, kwani nchi yako umeiangamiza, nao walio ukoo wako umewaua. Uzao wao wasiomcha hautatajwa kale na kale.
21
Watu husema: Na tuwatengenezee wana wao pa kuwachinjia kwa ajili ya manza, baba zao walizozikora, wasije kuinuka tena na kutwaa nchi na kupajaza hapa juu nchini miji yao!
22
Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Nitawainukia, niling'oe jina la Babeli nalo sao lake, wanawe na wajukuu; ndivyo, asemavyo Bwana.
23
Nitaiweka nchi yao kuwa kao lao nungu, iwe yenye mabwawa ya matopetope tu; nitapazoa kabisa na kutumia kizoleo kiangamizacho! Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
24
Bwana Mwenye vikosi ameapa kwamba: Kama nilivyoyawaza moyoni, yatakuwa vivyo hivyo; kama nilivyokata shauri, yatatimia vivyo hivyo.
25
Nitawaponda Waasuri katika nchi yangu, nitawamaliza na kuwakanyagakanyaga mlimani kwangu. Mizigo yao iondoke kwao wanaokaa kule, hata miti ya kuchukulia mizigo iondoke kwao mabegani.
26
Hili ndilo shauri, alilozipigia nchi zote; kwa hiyo mkono wake uko umewakunjukia wamizimu wote.
27
Kwani Bwana Mwenye vikosi akikata shauri, yuko nani atakayelitangua? Yuko nani atakayeukunja mkono wake uliokunjuka?
28
Mwaka ule, mfalme Ahazi alipokufa, tamko hili zito likatokea:
29
Ninyi wa nchi nzima ya Ufilisti, msifurahie kwamba: Fimbo iliyotupiga imevunjika! Kwani kooni mwa nyoka atatoka pili, naye atazaa nondo mwenye mabawa.
30
Hapo ndipo, wanyonge waliosongeka sana watakapolisha, nao wakiwa watalala hapohapo na kutulia vizuri; lakini mizizi yako nitaifisha kwa njaa, nao watakaosalia atawaua yule nondo.
31
Piga kilio, wewe lango! Omboleza, wewe mji! Zimia, nchi nzima ya Ufilisti! Kwani uko moshi utakaotoka kaskazini, kwao asiwe atakayeachwa peke yake kambini.
32
Nao majumbe wa taifa la kimizimu watapata jibu gani? Ni hili: Bwana ameushikiza Sioni! Wanyonge wao walio ukoo wake watapakimbilia!
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66