bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 29
Isaiah 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 30 →
1
Umekwisha kuapizwa, wewe Simba wa Mungu! Wewe Simba wa Mungu! Wewe mji, Dawidi alimotua! Ongezeni mwaka kwa mwaka na kula sikukuu miaka mizima!
2
Kisha nitamsonga Simba wa Mungu, kuweko kipiga kite na kuugua; ndipo, atakapokuwa mbele yangu Simba wa Mungu wa kweli.
3
Ndipo, nitakapokupigia makambi, yakuzinge, kisha nitakujengea boma la kukusonga, nitaisimamisha hata minara, nipate kukushinda.
4
Hapo ndipo, utakaponyenyekea, useme na kulala chini, maneno yako, utakayonitolea toka mavumbini, yatakuwa ya kujipunguza, sauti yako itakuwa kama ya mzimu atokaye kuzimuni, maneno yako ya kusema uvumbini yatakuwa ya kunong'ona tu.
5
Lakini mavumo ya wale wageni waliokujia yatakuwa kama mavumbi membamba, kweli mavumo ya hao wakorofi yatakuwa kama makapi yapeperushwayo; nayo yatakuwa kwa ghafula, wagunduliwe nayo.
6
Maana utakaguliwa na Bwana Mwenye vikosi, atakapokujia na kuitetemesha nchi kwa ngurumo, kwani ni mwenye sauti kuu, ataleta nao upepo wa kimbunga ulio wenye nguvu na ndimi za moto ulao.
7
Yatakuwa kama ndoto, mtu aliyoiota usiku, hayo mavumo ya wamizimu waliokuja kumshambulia Simba wa Mungu nao waliolipigia boma lake vita na kumsonga.
8
Itakuwa kama mwenye njaa anayeota akila chakula, lakini anapoamka hakuna kitu kwake, au kama mwenye kiu anayeota akinywa, lakini anapoamka hutweta na kuivuta roho yake. Hivyo ndivyo, yatakavyokuwa mavumo ya wamizimu wote, waliokuja kuushambulia mlima wa Sioni!
9
Tumbueni macho na kuyakodoa! Yatieni giza na kupofuka! Wamelewa, lakini si kwa mvinyo, wanapepesuka, lakini si kwa kileo.
10
Kwani Bwana amewamwagia ninyi roho ya usingizi mwingi, akayafumba macho yenu, ninyi wafumbuaji, akavifunika vichwa vyenu, ninyi wachunguzaji.
11
Hayo yote mliyoyaona yakawa kwenu kama maneno ya kitabu kulichofungwa na kutiwa muhuri; kama ajuaye kusoma anapewa na kuambiwa: Kisome hiki! atajibu: Siwezi, kwani kimefungwa na kutiwa muhuri.
12
Kama asiyejua kusoma anapewa na kuambiwa: Kisome hiki! atajibu: Sijui kusoma.
13
Bwana akasema: Ukoo huu hunikaribia na vinywa vyao, huniheshimu kwa midomo tu, lakini mioyo yao inanikalia mbali; kwa sababu hii hunicha bure, kwani hufundisha mafundisho yaliyo maagizo ya watu tu.
14
Kwa hiyo na mwone, ninavyoendelea kuufanyizia ukoo huu mambo ya mataajabu na ya vioja, werevu wao walio werevu wa kweli kwao upotee, nao utambuzi wa watambuzi wao usionekane.
15
Yatawapata wao walao njama, kwamba: wamfiche Bwana mashauri yao! Nao wafanyao gizani kazi zao na kusema: Yuko nani anayetuona? Yuko nani anayetujua?
16
Mmepotea kabisa! Uko udongo unaowaziwa kuwa sawa na mfinyanzi? Au kiko kiumbe kiwezacho kumwambia aliyekiumba: Hukunifanya? Au kiko chombo kiwezacho kumwambia aliyekifinyanga: Hujui kitu?
17
Sicho kitambo kidogo bado, Libanoni kugeuke kuwa shamba, nayo mashamba yawaziwe kuwa mwitu?
18
*Siku ile viziwi watayasikia maneno yaliyoandikwa, nayo macho ya vipofu yaliyokuwa yenye giza jeusi yataona.
19
Nao wanyonge wataendelea kumfurahia Bwana nao walio wakiwa kuliko watu wengine watamshangilia Mtakatifu wa Isiraeli.
20
Kwani wakorofi watakuwa wamekwisha, nao wafyozaji watakuwa wameangamia, nao wote watakuwa wameng'olewa waliokataa kulala usingizi, wapate kuwapotoa wenzao.
21
Ndio wanaokosesha wengine shaurini, ndio wanaowategea waamuliao penye malango ya mji, kwani hivyo wanawapotoa waongofu, wasishinde shaurini.*
22
Kwa sababu hii Bwana alimkomboa Aburahamu, akauambia mlango wa Yakobo: Sasa Yakobo hatapatwa tena na soni, wala uso wake hautamvilia tena.
23
Kwani watoto wake watakapoona, mikono yangu itakayoyafanya kwao, watalitakasa Jina langu, ndiko kumtakasa Mtakatifu wa Yakobo na kumcha Mungu wa Isiraeli.
24
Ndipo, waliopotea rohoni watakapojua utambuzi nao walionung'unika watajifundisha yafaayo.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66