bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 30
Isaiah 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 31 →
1
Ndivyo, asemavyo Bwana: Yatawapata wale wana wabishi wapigao shauri lisilo la kwangu, wafanyao agano pasipo Roho yangu, kusudi waongeze kosa kwa kosa.
2
Ndio wanaokwenda kushuka Misri pasipo kukiuliza kinywa changu, wajipatie nguvu kwa nguvu za Farao kwa kukikimbilia kivuli cha Misri.
3
Lakini nguvu zake Farao zitawageukia, ziwatie soni, nako kukikimbilia kivuli cha Misri kutawapatia matusi.
4
Ijapo wakuu wake waje Soani, ijapo wajumbe wake wafike mpaka Hanesi,
5
wao wote wataona soni na watu wasiowafalia kitu, kwa kuwa hawawezi kuwasaidia au kuwapatia cho chote kuwafaliacho, kwani wanawatia soni tu, wengine wawabeze na kuwatukana. Tamko zito lililotoka kwa ajili ya nyama wa kusini:
6
Wanapita katika nchi yenye masongano na mahangaiko, kwani wamo simba na chui, pili na nyoka za moto warukao. Huko wanapitisha mali zao migongoni kwa punda, nako kwenye nundu za ngamia malimbiko yao, wayapelekee watu wasiowafalia kitu.
7
Nayo Misri msaada wake ni kama mvuke, ni wa bure tu, kwa sababu hii waliipa jina hili: Mkuu wa maneno anayejikalia tu.
8
Sasa nenda, uyachore katika kibao machoni pao, kisha uyaandike namo kitabuni, siku za nyuma yapate kuwashuhudia kale na kale.
9
Kwani ndio watu wabishi na wana wenye uwongo, kweli ndio wana wasiotaka kuyasikia Maonyo ya Bwana.
10
Huwaambia waonaji: Msione! nao watazamaji: Msitutazamie yaliyo ya kweli! Sharti mtuambie yaliyo mafuta ya midomo, sharti mtutazamie madanganyifu!
11
Ondokeni njiani penye kweli! Ipotoeni mikondo inyokayo! Tuacheni, tupumzike, tusimwone Mtakatifu wa Isiraeli!
12
Kwa hiyo Mtakatifu wa Isiraeli anasema: Kwa kuwa mmelikataa neno hili, mkayaegemea mambo yenye ukorofi na upotovu, mkayatumia ya kujishikizia:
13
kwa sababu hii hizo manza, mlizozikora, zitakuwa kama ufa unaokwenda ukipanuka katika ukuta mrefu, nao utabomoka ghafula na kuwagundua watu.
14
Naye Bwana atauvunja, kama watu wanavyovunja mtungi wakiupigapiga pasipo kuuhurumia, hapo, utakapovunjika, kisipatikane kigae cha kupalia moto jikoni, wala cha kutekea maji kisimani.
15
Kwani hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu, aliye Mtakatifu wa Isiraeli: Mtakaporudi na kutulia, mtaokolewa; mtakaponyamaza na kujiegemeza, mtapata nguvu, lakini mmekataa!
16
Mkasema: Hapana! Na tupande farasi, tupige mbio! Kwa hiyo mtakimbia. Mkasema: Na tupande farasi wenye mbio sana! Kwa hiyo watakaowafukuza watawapigisha mbio.
17
Elfu wa kwenu wataikimbia yowe ya mmoja; watano wakipiga yowe, mtakimbia wote, mpaka masao yenu yawe kama mlingoti ulioko mlimani juu au kama bendera iliyoko kilimani.
18
Kwa hiyo Bwana anangoja, apate kuwatolea upole; kwa hiyo anainuka, apate kuwahurumia, kwani Bwana ni Mungu wa kuamua kweli; wenye shangwe ni wote wanaomngoja,
19
kwani walio wa Sioni watakaa Yerusalemu. Hamtalia machozi kamwe, atawaendea kwa upole; atakapozisikia sauti za vilio vyenu atawaitikia.
20
Kweli, Bwana amewalisha mikate ya masongano, akawanywesha maji ya mahangaiko, lakini wafunzi wako hawatajificha tena, ila macho yako yatakuwa yakiwatazamia wafunzi wako.
21
Nayo masikio yako yatasikia neno litokalo nyuma yako kwamba: Njia ni hii, ishikeni! kama mtakuwa mmeiacha kuumeni au kushotoni.
22
Hapo ndipo, mtakapovichafua vinyago vyenu vya miti vilivyofunikwa na fedha navyo vilivyofunikwa na dhahabu, utavitupatupa, kama ni takataka, na kuviambia: Tokeni kwetu!
23
Naye atakupa mvua za mbegu zako, ulizozipanda shambani, nalo shamba litakutolea mikate itakayokuwa yenye nguvu ya kunonesha, nao kondoo wako watalisha siku zile kwenye uwanda mpana.
24
Nao ng'ombe na punda wako wanaolima shamba watakula muhindi ulioungwa na majani yenye chumvi, nao utakuwa umepepetwa kwa ungo na kipepeto.
25
Katika kila mlima mrefu, hata katika kila kilima kiendacho juu kutakuwa na vijito vya maji yarukayo; itakuwa siku ile, wengi watakapouawa, minara itakapoanguka.
26
Nao mwanga wa mwezi utakuwa kama wa jua, nao mwanga wa jua utaongezeka mara saba, uwe kama wa siku saba. Itakuwa siku ile, Bwana atakapovifunga vidonda vyao walio ukoo wake na kuyaponya machubuko, aliyowapiga.
27
Tazameni, Jina la Bwana linakuja toka mbali, makali yake yanawaka, moshi mwingi unapanda, midomo yake imejaa machafuko, ulimi wake ni kama moto ulao!
28
Pumzi yake ni kama mto udidimizao, nayo maji yake hufika shingoni, awapepete wamizimu katika pepeto liangamizalo, atie mataifa mazima hatamu vinywani za kuwapoteza.
29
Nanyi mtaimba, kama watu wanavyoimba katika usiku wa kuandalia sikukuu, mtafurahi mioyoni kama wasafiri wanaokwenda na kupiga mazomari, waje mlimani kwa Bwana aliye mwamba wa Isiraeli.
30
Ndipo, Bwana atakapoipaza sauti yake yenye utukufu, atauonyesha nao mkono wake, jinsi unavyokunjuka, akifoka kwa ukali na kuwakisha ndimi za moto ulao, akileta kimbunga na mvua yenye maji mengi pamoja na mvua ya mawe.
31
Kwani Waasuri watastushwa na sauti yake Bwana, atakapowapiga kwa fimbo yake:
32
kila mara fimbo ya kuwapiga itakapotokea, Bwana akiielekeza, iwajie, itakuwa kwa kupiga patu na mazeze, vita vyake vitakuwa hivyo akiwatisha na kuwapigapiga.
33
Kwani tangu kale pametengenezwa mahali pa kuchinjia watu, wawe ng'ombe za tambiko, naye mfalme amepatengenezewa pake, napo ni papana na parefu kwenda chini; kuzunguka hapo moto uko tayari, hata kuni nyingi zimekwisha kupangwa; pumzi ya Bwana yenye moto wa kiberitiberiti itaziwasha.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66