bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 7
Isaiah 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 8 →
1
Siku za Ahazi, mwana wa Yotamu, mwana wa Uzia, alipokuwa mfalme wa Yuda, ndipo, Resini, mfalme wa Ushami, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Isiraeli, walipokuja kupiga vita nao waliomo Yersalemu, lakini hawakuweza kuwashinda vitani.
2
Walio wa mlango wa Dawidi walipopashwa habari, ya kwamba vikosi vya Washami vimeingia katika nchi ya Efuraimu, vikapiga makambi, mioyo yao ikatikisika nayo mioyo ya watu wao, kama miti ya mwituni inavyotikiswa na upepo.
3
Lakini Bwana akamwambia Yesaya: Toka wewe na mwanao Seari-Yasubu (Sao litarudi), uje kukutana na Ahazi, mwishoni pa mfereji wa maji ya ziwa la juu, kule barabarani panapokwenda kwenye shamba la Mfua nguo.
4
Mwambie: Jiangalie, utulie, usiogope! Jipe moyo kwa ajili ya moshi wa hivyo vijinga viwili vilivyomo katika kuzimika, ijapo makali ya Resini na ya Washami na ya mwana wa Remalia yawakishe moto.
5
Kweli Washami, Waefuraimu na mwana wa Remalia wamekulia njama mbaya ya kwamba:
6
Na tupande kwenda Yuda, tuwastushe tukiwashambulia na kuwashinda, kisha tumweke mwana wa Tabeli kuwa mfalme kwao katikati!
7
Kwa sababu hii Bwana Mungu anasema: Hayatatimia! Hayatakuwa!
8
Kwani kichwa cha Ushami ni Damasko, nacho kichwa cha Damasko ni Resini, tena miaka 65 itakapopita, Efuraimu atakuwa amepondwa kabisa, wasiwe ukoo tena.
9
Kichwa cha Efuraimu ni Samaria, nacho kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia. Ikiwa mnakosa wa kumtegemea, kweli hamtategemezwa.
10
Bwana akaendelea, akamwambia Ahazi kwamba:
11
Jiombee kielekezo kwake Bwana Mungu wako! Omba kilicho mbali kuzimuni au kilicho mbali mbinguni!
12
Ahazi akajibu: Sinacho nitakachokiomba, nisimjaribu Bwana.
13
Ndipo, (Yesaya) aliposema: Sikilizeni, ninyi mlio wa mlango wa Dawidi! Je? Havijawatoshea kuwachokoza watu, mkimchokoza naye Mungu wangu?
14
Kwa hiyo Bwana atawapa mwenyewe kielekezo, ni hiki: Tazama, mwanamwali atapata mimba, atazaa mtoto mwanamume, nalo jina lake atamwita Imanueli (Mungu yuko nasi).
15
Atakula maziwa yenye mafuta na asali, mpaka atakapojua kukataa mabaya na kuchagua mema.
16
Yule kijana atakapokuwa hajajua bado kukataa mabaya na kuchagua mema, nchi ile itakuwa imeachwa, sasa unawastukiaje wafalme wake wawili?
17
Bwana atawaletea ninyi, wewe nao wa ukoo wako nao wa mlango wa baba yako, siku zisizokuja bado kuanzia siku ile, Waefuraimu walipojitenga kwao Wayuda; itakuwa hapo, mfalme wa Asuri atakapokuja.
18
Siku ile mbung'o walioko mwishoni kwenye mito ya Misri nao nyuki walioko katika nchi ya Asuri Bwana atawapigia miluzi, waje.
19
Watakuja kutua wote pamoja katika mabonde na makorongo, katika nyufa za magenge, hata katika maboma yote ya miti yenye miiba na malishoni po pote.
20
Siku ile Bwana atamtumia mfalme wa Asuri kuwa kama wembe uliokopwa ng'ambo ya lile jito kubwa, awanyoe nywele za vichwa na za miguu, hata za ndevu zitamalizwa zote pia.
21
Siku ileile mtu atafuga king'ombe kimoja na vibuzi viwili tu.
22
Lakini kwa kupata maziwa mengi kwao hao atakula mafuta; wote watakaosalia katika nchi hiyo watakula mafuta na asali.
23
Tena siku ile kila mahali penye mizabibu elfu iletayo sasa fedha elfu patakuwa penye mikunju na mibigili.
24
Watu wakienda mahali kama hapo watashika mishale na pindi, kwani nchi nzima itakuwa mapori yenye mikunju na mibigili.
25
Nako kwenye milima kote kunakolimwa sasa na majembe, watu hawatakwenda tena huko kwa kuiogopa mikunju na mibigili, watakutumia tu kwa kuchungia ng'ombe na kondoo na mbuzi, wachezeechezee kuko huko.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66