bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 5
Isaiah 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 6 →
1
Na niimbe mambo ya mpendwa wangu! Ni wimbo wa mpenzi wangu wa kuiimbia mizabibu yake. Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu penye kilima kilichoiotesha sana.
2
Akalima na kuchimba, hata mawe akayaokota, akapanda mizabibu mizuri akajenga dungu katikati, akachimbua nalo kamulio kwake; kisha alingoja, izae zabibu, lakini ikazaa mbaya zisizolika.
3
Sasa ninyi mkaao Yerusalemu nanyi waume wa Yuda, tuamulieni mimi na mizabibu yangu!
4
Yako mambo gani ya kuifanyizia mizabibu, nisiyoifanyizia? Mbona nilikaa na kuzingojea zabibu, ikanizalia tu zisizolika?
5
Sasa na niwajulishe, mimi nitakayoifanyizia mizabibu yangu: nitaliondoa boma lao, iwe malisho, nitakibomoa kitalu chao, ife kwa kukanyagwa.
6
Nitaiacha, iwe pori lenyewe, isipogolewe wala isilimiwe, pakue mikunju na mibigili; kisha nitayaagiza mawingu, yasiinyeshee mvua.
7
Kwani mizabibu ya Bwana Mwenye vikosi ni mlango wa Isiraeli na watu wa Yuda, ndio shamba lake lipendwalo naye. Akangojea manyofu, lakini alipotazama, ni mapotovu; akangojea wongofu, lakini alipotazama, ni vilio tu.
8
Yatawapata wanaokusanya nyumba na nyumba ndio wanajiongezea mashamba na mashamba, pasiwepo tena mahali pasipo penu, mkae peke yenu katika nchi.
9
Masikioni mwangu limo neno la Bwana Mwenye vikosi: Kweli nyumba nyingi zitakuwa mahame, ijapo ziwe kubwa na nzuri, asipatikane mtu wa kukaa humo.
10
Kwani mashamba kumi ya mizabibu yatatoa kibuyu kimoja tu, kikapu kizima cha mbegu kitaleta pishi moja tu.
11
Yatawapata waamkao mapema wakijitafutia vileo nao wakaao mpaka usiku kwenye pombe na kuvimbisha vichwa.
12
Hapo wanyweapo yako mazeze na mapango, hata matoazi na mazomari, lakini kazi za Bwana hawazitazami, wala matendo ya mikono yake hawayaoni.
13
Kwa hiyo wao walio ukoo wangu watatekwa wakiwa hawajui maana, watukufu wao watakuwa wenye njaa, nao walio watuwatu tu watazimia kwa kiu.
14
Kwa hiyo kuzimu kutakuwa kumejipanua na kukifumbua kinywa chake pasipo mpaka, watukufu wa Sioni pamoja na watu wake wapate kushuka nao waliochezacheza mle na kupiga vigelegele vya furaha.
15
Hapo watu watainamishwa, nao waume watanyenyekezwa, hayo macho yenye majivuno yatanyenyekezwa.
16
Lakini Bwana Mwenye vikosi atatukuka kwa kunyosha maamuzi, yeye aliye Mungu mtakatifu atajulika kwa wongofu kuwa Mtakatifu kweli.
17
Wana wa kondoo watalisha hapo, kama ni malisho yao, nako kwenye mahame ya wale wakwasi watakula wageni.
18
Yatawapata wajivutiao mabaya kwa vigwe vya udanganyifu, tena makosa kwa kamba za magari.
19
Ndio wanaosema: Na apige mbio, afanye upesi matendo yake, tuyaone! Shauri lake Mtakatifu wa Isiraeli na litimie na kutokea, tulitambue!
20
Yatawapata wanaosema: Kibaya ni chema nacho chema wanakiita kibaya. Giza huigeuza kuwa mwanga, nao mwanga huugeuza kuwa giza. Machungu huyageuza kuwa matamu, nayo matamu huyageuza kuwa machungu.
21
Yatawapata wanaojiwazia wenyewe kuwa werevu wa kweli na watambuzi.
22
Yatawapata walio wenye nguvu za kunywa pombe, walio na ufundi wa kuchanganya vileo.
23
Kwa kupenyezewa mali huwashindisha wapotovu shaurini, lakini wongofu wao waongokao huutengua, wasishinde!
24
Kwa hiyo watakuwa hivyo: kama ndimi za moto zinavyokula mabua, au kama majani makavu yanavyojipinda motoni, ndivyo, mizizi yao itakavyobunguka, nayo maua yao yatapeperushwa kama mavumbi, kwani waliyakataa Maonyo yake Bwana Mwenye vikosi, wakalibeza Neno lake Mtakatifu wa Isiraeli!
25
Kwa hiyo Bwana akawachafukia walio ukoo wake, mkono wake ukawainamia, ukawapiga; milima ikatetemeka, mizoga yao ikawa kama mataka njiani. Kwa hayo yote makali yake hayajatulia bado, mkono wake ungaliko umekunjuka bado.
26
Atatweka bendera ya kuwaitia wamizimu wakaao mbali nao wakaao kwenye mapeo ya nchi atawapigia mbiu, na mwaone, wakija na kupiga mbio sana.
27
Mwao hao hamna mchovu ajikwaaye mara kwa mara, wala hamna apendaye kusinzia wala kulala usingizi, wala hamna mwenye mshipi kiunoni ufungukao, wala hamna mwenye viatu vikatikavyo mikanda.
28
Mishale yao itakuwa imenolewa, nyuta zao zitakuwa zimepindwa, kwato za farasi wao zitaonekana kuwa ngumu kama mawe, magurudumu ya magari yao yatapiga mbio kama upepo mkali.
29
Mazomeo yao ni kama ngurumo ya simba, hulia kama wana wa simba. Watakuja na kuvuma na kukamata mateka, wayapeleke kwao; napo hapo hatakuwapo atakayewaponya.
30
Makelele, watakayowapigia siku ile, yatakuwa kama maumuko ya mawimbi ya bahari; kama mtaichungulia nchi, itakuwa yenye giza la kuogopesha, mwanga utakuwa umegeuka giza kwa weusi wa mawingu yaliyoko juu yake.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66