bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 24
Isaiah 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 25 →
1
Tazameni, Bwana anaondoa watu katika nchi, iwe peke yake! Anaiumbua umbo lake na kuwatawanya wanaokaa huku.
2
Wote watakuwa sawa: watu na mtambikaji, mtumwa na mabwana wake, kijakazi na bibi yake, anunuaye na auzaye, akopeshaye na akopaye, mwenye kudai na mwenye kudaiwa.
3
Kweli nchi itaondolewa watu kabisa, nazo mali zitapokonywa, kwani Bwana amelisema neno hilo.
4
Nchi imesikitika, maana imenyauka, ulimwengu wote umefifia, maana umenyauka, nao walio wakuu wa watu katika nchi wamefifia.
5
Chini yao wakaao huku nchi imechafuliwa, kwani wameyapita Maonyo, hawakuyafuata maongozi, wakalivunja Agano la kale na kale.
6
Kwa sababu hii apizo limeila nchi; nao wakaao huku wanalipishwa manza, walizozikora; kwa sababu hii waikaao nchi wameunguzwa, watu waliosalia ni wachache tu.
7
Mvinyo mbichi zimesikitika, mizabibu imefifia, wote waliokuwa na furaha mioyoni hupiga kite.
8
Patu zilizofurahisha hunyamaza, makelele yao wapigao vigelegele yamekoma, nayo mazeze yaliyofurahisha hunyamaza.
9
Hawanywi tena mvinyo na kuiimbia, kileo cha sasa ni chenye uchungu kwao wanaokinywa.
10
Mji umebomolewa, uko peke yake tu, kila nyumba imefungwa, hakuna anayekuja.
11
Makelele ya kulilia mvinyo yanasikilika huko nje, furaha yote imeguiwa na giza, maana yote yaliyoifurahisha nchi yamehama.
12
Yaliosalia mjini ni mahame tu, nalo lango lake limevunjwavunjwa kuwa vipandepande tu.
13
Kwani hivyo ndivyo, mambo yatakavyokuwa katika nchi katikati ya watu, kama yalivyo penye mavuno ya matunda ya mchekele au penye kuokoteza, mavuno ya zabibu yakiisha.
14
Hawa wanapaza sauti zao kwa kupiga vigelegele wakiushangilia utukufu wa Bwana kuanzia baharini.
15
Kwa hiyo mtukuzeni Bwana nako maawioni kwa jua, nako kwenye visiwa vilivyoko baharini litukuzeni Jina la Bwana Mungu wa Isiraeli!
16
Toka mapeoni kwa nchi tulisikia nyimbo kwamba: Mwongofu na apambwe! Nikajibu kwamba: Ni mnyonge! Ni mnyonge! Nimekufa! Wakorofi wanakorofisha, kweli wakorofi wanakorofisha kwa ukorofi.
17
Mastuko na miina na matanzi yanawangoja ninyi mkaao katika nchi!
18
Itakuwa hivi: Atakayeyakimbia makelele ya kustusha ataanguka mwinani, naye atakayepanda na kutoka mwinani atanaswa na tanzi, kwani madirisha ya huko juu yatakuwa yamefunguliwa, nayo misingi ya nchi itatetemeka.
19
Nchi itavunjikavunjika, nchi itaatukaatuka, nchi itayumbayumba.
20
Nchi itapepesukapepesuka kama mlevi, itachukuliwa huko na huko kama machela, italemewa na mapotovu yake, itaanguka, isiweze kuinuka tena.
21
Siku ile itakuwa hivi: Bwana atavijilia vikosi vya juu huko juu, nao wafalme wa nchi atawajilia huku chini.
22
Watakusanywa, kama wafungwa wanavyokusanywa, wapelekwe shimoni, wafungwe kifungoni, tena wafunguliwe, siku nyingi zitakapopita.
23
Hapo ndipo, mwezi utakapojifunika, ndipo, nalo jua litakapoona soni, kwa kuwa Bwana Mwenye vikosi atakuwa yuko mfalme mlimani kwa Sioni namo Yerusalemu, nako mbele ya wazee wake utakuwako utukufu.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66