bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 60
Isaiah 60
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 59
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 61 →
1
*Inuka uangazike! Kwani mwanga wako unakuja, nao utukufu wa Bwana umekuzukia.
2
Kwani tunapotazama, giza linaifunika nchi, mawingu meusi yanayafunika makabila ya watu, lakini wewe, Bwana anakuzukia, nao utukufu wake unaonekana juu yako.
3
Wamizimu wataujia mwanga wako, nao wafalme wataujia mmuliko uliozuka kwako.
4
Yainue macho yako, utazame po pote! Hao wote wamekusanyika, waje kwako; wanao wa kiume watakuja, wakitoka mbali, wanao wa kike wataletwa na kubebwa.
5
Utakapowaona utachangamka, nao moyo wako utapigapiga, upanuke, kwani mafuriko ya bahari yatageuka, yaje kwako, nayo mapato ya wamizimu yataingia kwako.
6
Makundi ya ngamia yatakufunika, hata vijana wa ngamia wa Midiani na wa Efa, wote watatoka Saba, waje kwako, wakichukua dhahabu na uvumba, nao watamtangaza Bwana na kumshangilia.*
7
Makundi yote ya Kedari, yale ya mbuzi na ya kondoo yatakusanyika kwako, madume ya Nebayoti utayatumia ya tambiko, yatanipendeza juu ya meza ya kunitambikia; ndivyo, nitakavyoitukuza Nyumba ya utukufu wangu.
8
Hao ni wa nani wanaoruka kama mawingu au kama hua wanaoyarukia matundu yao?
9
Kwani visiwa vinaningojea, nazo merikebu za Tarsisi zitakuwa za kwanza za kuwaleta wanao toka nchi za mbali; fedha zao na dhahabu zao wanazo za kulitolea Jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa yeye aliye Mtakatifu wa Isiraeli amekupa utukufu.
10
Wana wa nchi ngeni watalijenga boma lako, nao wafalme wao watakutumikia, kwani nilipokuchafukia nilikupiga, tena nilipopendezwa nawe nimekuhurumia.
11
Malango yako yatakuwa wazi siku zote, hayatafungwa mchana wala usiku, wakuletee mapato ya wamizimu, nao wafalme wao watajitia mumo humo.
12
Kwani kila taifa na kila nchi ya kifalme itakayokataa kukutumikia itaangamia, nao watu wao watatoweka kabisa.
13
Utukufu wa Libanoni utakuja kwako, mivinje na mitamba na mizambarau yote pamoja iwe mapambo ya mahali pangu patakatifu, maana mahali, miguu yangu itakapopakanyaga, nitapapatia marembo.
14
Nao wana wao waliokutesa watakuja kwako na kuinama chini, nao wote waliokutukana watakuangukia penye nyayo za miguu yako, watakuita mji wa Bwana, Sioni wa Mtakatifu wa Isiraeli.
15
Kwa sababu ulikuwa umeachwa, ukachukizwa, watu wakakataa kupitia kwako, kwa hiyo nitakuweka kuwa mahali pa kujivunia kale na kale, tena kuwa wa kufurahisha vizazi na vizazi.
16
Utanyonya maziwa ya mataifa mengine, kweli vifuani kwa wafalme utanyonya, kwani mimi Bwana ni mwokozi wako, mkombozi wako ni yeye amtawalaye Yakobo.
17
Penye shaba nitaleta dhahabu, penye vyuma nitaleta fedha, penye miti nitaleta shaba, penye mawe nitaleta vyuma. Nitaweka utengemano kuwa ukuu wako nao wongofu kuwa ubwana wako.
18
Hayatasikiwa tena makorofi katika nchi yako, wala hayatasikilika maangamizo na mavunjiko katika mipaka yako. Boma lako utaliita Wokovu, nayo malango yako utayaita Mashangilio.
19
Halitawaka tena jua kwako kuwa mwanga wa mchana, wala mwezi hautakumulikia tena, upate kuona, kwani Bwana atakuwa mwanga wako kale na kale, Mungu wako atakuwa utukufu wako.
20
Jua lako halitakuchwa tena, wala mwezi wako hautakufa tena, kwani Bwana atakuwa mwanga wako wa kale na kale, nazo siku zako za kusikitika zitakuwa zimekwisha.
21
Walio wa ukoo wako wote watakuwa waongofu, watakuwa wenye nchi kale na kale, kwa kuwa ni shamba, nililolipanda, ni kazi ya mikono yangu, nijipatie matukuzo.
22
Aliye mdogo atageuka kuwa elfu, naye aliye mnyonge atageuka kuwa taifa lenye nguvu. Mimi Bwana nitayafanyiza upesi, siku zake zitakapotimia.
← Chapter 59
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 61 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66