bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 66
Isaiah 66
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 65
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
1
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mbingu ni kiti changu cha kifalme, nayo nchi ni pa kuiwekea miguu yangu. Ni nyumba gani, mtakayonijengea? Tena mahali pa kupumzikia mimi ni mahali gani?
2
Hayo yote mkono wangu uliyafanya, yakawapo hayo yote; ndivyo, asemavyo Bwana. Ninaowatazama, ndio wakiwa nao wapondekao rohoni, nao wanaotetemeka wakalisikia Neno langu.
3
Achinjaye ng'ombe huwa kama mwenye kuua mtu, naye atoaye kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko huwa kama mwenye kunyonga mbwa, naye atoaye vyakula kuwa vipaji vya tambiko humwaga nazo damu za nguruwe, avukizaye uvumba hutambikia mizimu: hao ndio waliojichagulia njia zao, nazo roho zao zikapendezwa na matapisho yao.
4
Ndivyo, nami nitakavyojichagulia masumbufu ya kuwasumbua, nayo matisho, waliyoyaogopa, nitayaleta kwao, kwa kuwa nilipowaita, hawakujibu; niliposema, hawakusikia, wakayafanya yaliyokuwa mabaya machoni pangu, wakayachagua, ambayo nilikuwa zipendezwi nayo.
5
Lisikilizeni Neno la Bwana, mtetemekao mkilisikia Neno la Bwana! Ndugu zenu wanaowachukia ninyi, waliowafukuza kwa ajili ya Jina langu walisema: Bwana na autokeze utukufu wake, tuone, mkiufurahia! Lakini wao watapatwa na soni.
6
Usikilizeni uvumi uliomo mjini, uliomo namo Nyumbani mwa Bwana! Ni sauti ya Bwana anayewalipisha adui matendo yao.
7
Alipokuwa hajashikwa na uchungu bado amezaa, alipokuwa hajaumwa bado amepata mtoto wa kiume.
8
Yuko nani aliyesikia kama hayo? Yuko nani aliyeona kama hayo? Inakuwaje, nchi ikitokezwa siku moja? Inakuwaje, ukoo mzima wa watu ukizaliwa kwa mara moja? Kwani Sioni uliposhikwa na uchungu papo hapo umewazaa watoto wake.
9
Je? Mimi nifikishe watoto pa kuzaliwa, nisiwazalishe? ndivyo, Bwana anavyosema. Je? Mimi ninapozalisha, nilifunge tumbo la mama? ndivyo, Mungu wako anavyosema.
10
Changamkeni pamoja na Yerusalemu! Ushangilieni, nyote mwupendao! Furahini pamoja nao furaha kuu, nyote mliousikitikia!
11
Kwa maana mtayanyonya na kushiba maziwa yake yenye matulizo ya moyo! Kwa maana mtanyonya na kukamua, mjipendezeshe kwa mfuriko wa utukufu wake.
12
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Tazameni! Nitauelekeza utengemano, ufike kwake ukiwa kama mto mkubwa, nayo matukufu ya wamizimu nitayalekeza, yafike kwake yakiwa kama kijito kifurikacho maji. Nanyi mtanyonya mkibebwa vifuani, mtabembelezwa na kuwekwa magotini.
13
Kama mama anavyoutuliza moyo wa mtoto wake, ndivyo, nami nitakavyoituliza mioyo yenu; namo Yerusalemu ndimo, mtakamotulizwa mioyo yenu.
14
Mtakapoyaona, mioyo yenu itafurahi, nayo mifupa yenu itachipuka kama majani mabichi, nao mkono wake Bwana utajulikana kwa watumishi wake, nayo makali yake yatajulikana kwa adui zake.
15
Kwani na mwone, Bwana anavyokuja motoni, magari yake yakikimbizwa na upepo mkali, awalipe kwa moto wa makali yake na kwa mavumo ya moto uwakao na nguvu.
16
Kwani Bwana atawapatiliza wote wenye miili ya kimtu kwa moto na kwa upanga, nao watakaouawa naye Bwana watakuwa wengi.
17
Wajitakasao na kujeulia matambiko ya shambani wakimfuata mtambikaji alioko kati yao, nao walao nyama za nguruwe nazo za kibudu na za panya, wote pamoja watatoweshwa; ndivyo, asemavyo Bwana.
18
Nami ninayajua matendo yao na mawazo yao; patakuja, nitakapoyakusanya mataifa na misemo yote ya watu, nao watakuja, wauone utukufu wangu.
19
Ndipo, nitakapowafanyizia kielekezo, nao waliookoka kwao wengine nitawatuma kwenda kwa wamizimu wa Tarsisi nako kwao wa Pulu na wa Ludu walio mafundi wa kupinda pindi, nako kwao wa Tubali na kwa Wagriki, nako kwenye visiwa vilivyoko mbali. Hawa hawajasikia habari za kwangu, hawajauona bado utukufu wangu; watautangaza utukufu wangu kwao hao wamizimu.
20
Nao watawaleta ndugu zenu wote kuwa kipaji cha tambiko cha Bwana wakiwatoa kwenye mataifa yote; nao watapanda farasi na magari, wengine watachukuliwa katika machela, wengine watapanda nyumbu na ngamia, waje kufika Yerusalemu kwenye mlima wangu mtakatifu; ndivyo, Bwana anavyosema. Watawaleta hivyo, kama wana wa Isiraeli wanavyovipeleka vipaji vya tambiko Nyumbani mwa Bwana katika vyombo vilivyotakaswa.
21
Namo mwao nitachukua wengine, wawe watambikaji na Walawi; ndivyo, Bwana anavyosema.
22
Kwani kama zile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazoziumba, zitakavyokaa mbele yangu, ndivyo, mazao yenu na majina yenu yatakavyokaa; ndivyo, asemavyo Bwana.
23
Tena itakuwa, kila mara, mwezi utakapoandama, na kila mara, siku ya mapumziko itakapokutia, wote wenye miili ya kimtu watakuja kunitambikia; ndivyo, Bwana anavyosema.
24
Kisha watatoka mjini, waitazame mizoga ya watu walionitengua; kwani mdudu mwenye kuwaumiza hatakufa, wala moto wa kuwala hautazimika, nao watakuwa tapisho kwao wote walio wenye miili ya kimtu.
← Chapter 65
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66