bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 19
Isaiah 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 20 →
1
Tazameni: Bwana amepanda wingu jepesi, aje Misri! Vinyago vya Misri vinatikisika usoni pake, mioyo yao Wamisri imeyeyuka vifuani mwao.
2
Nitawachochea Wamisri, wapigane na Wamisri wenzao, wagombane mtu na ndugu yake, hata mtu na mwenziwe, hata mji upigane na mji mwingine, vilevile ufalme ugombane na ufalme mwingine.
3
Hapo ndipo, roho zao Wamisri zitakapozimia vifuani mwao, nikiitengua mizungu yao; nao watatafuta msaada kwa vinyago na kwa waganga, kwa wachawi na kwa waaguaji.
4
Nitawafungia Wamisri mikononi mwa bwana mgumu, mfalme, mwenye ukorofi, awatawale! Ndivyo, asemavyo Bwana aliye Bwana Mwenye vikosi.
5
Kisha maji yatakupwa baharini, nao mto mkubwa utakauka, pawe pakavu tu.
6
Mifereji mikubwa ya maji itanuka vibaya, nayo mito ya Misri ya chini itakuwa minyonge, kisha itakauka nayo, hata matete na manyasi yatanyauka.
7
Viwanda vilivyoko kando ya mto kwenye kingo za mto, nayo mashamba yote ya mtoni yatanyauka, yatakauka kabisa yatoweke.
8
Wavuvi watalia, pamoja nao wote waliokamata samaki mtoni kwa ndoana watasikitika, nao waliotanda nyavu majini watafifia.
9
Hata wafanyao kazi za pamba wataangamia pamoja nao wafumao nguo nyeupe.
10
Hivyo misingi yao itakuwa imepondeka, wote wafanyao kazi za kibarua wataumia rohoni.
11
Wakuu wa Soani watakuwa wamepumbaa kabisa; nao wajuzi wa Farao wasiokosa mizungu, hapo mizungu yao itakuwa ujinga tu. Mtawezaje kumwambia Farao: Mimi ni mwana wao watambuzi? au: Mimi ni mwana wao wafalme wa kale?
12
Sasa watambuzi wako wako wapi? Kama wanalitambua, na wakufumbulie shauri, Bwana Mwenye vikosi aliloikatia nchi ya Misri!
13
Wakuu wa Soani ni wajinga kweli, nao wakuu wa Nofu wamedanganyika, waliokuwa vichwa vya milango wameiangamiza Misri.
14
Bwana amemwaga mioyoni mwao roho za kizunguzungu, wawapoteze Wamisri katika matendo yao yote, wapepesuke kama mlevi kwenye matapiko yake.
15
Hakuna tendo tena, Wamisri, watakalolitenda, kama ni kichwa au mkia, kama ni makuti au majani.
16
Siku zile Wamisri watakuwa kama wanawake, watetemeke kwa kuyastukia matisho ya mkono wa Bwana Mwenye vikosi, atakaowakunjulia.
17
Hapo nchi ya Yuda itawawia Wamisri kitisho, kila mtu aingiwe na kituko atakaposikia, ikitajwa, kwa ajili ya shauri la Bwana Mwenye vikosi, alilowakatia.
18
Siku ile miji mitano itakuwako katika nchi ya Misri itakayosema msemo wa Kanaani, itakayoapa na kulitaja Jina la Bwana Mwenye vikosi, mmoja wao utaitwa Mji wa Mabomoko.
19
Siku zile patakuwako pa kumtambikia Bwana katika nchi ya Misri katikati na nguzo ya Bwana iliyojengwa kwa mawe mpakani kwake.
20
Hivyo Bwana Mwenye vikosi atakuwa na kielekezo cha kumshuhudia katika nchi ya Misri; napo, watakapomlilia Bwana kwa ajili yao wawasongao, atatuma mwokozi, awagombee, awaponye.
21
Ndivyo, Bwana atakavyojulikana kwa Wamisri, kweli Wamisri watamjua Bwana siku zile, watamtumikia na kumtolea ng'ombe za tambiko na vipaji vingine vya tambiko, nayo waliyomwagia Bwana kumpa, watayalipa.
22
Itakuwa hivyo: Bwana akiwapiga Wamisri na kuwaponya, nao wakimrudia Bwana, atawaitikia, wakimwomba, awaponye kabisa.
23
Siku zile itakuwako barabara toka Misri kwenda Asuri, nao Waasuri watakuja Misri, nao Wamisri watakuja Asuri kuamkiana, hivyo Wamisri na Waasuri watatumikiana.
24
Siku zile Isiraeli atakuwa wa tatu wa kupatana na Misri na Asuri, hawa watakuwa mbaraka katika nchi katikati.
25
Naye Bwana Mwenye vikosi atawabariki na kusema: Wabarkiwe Wamisri walio ukoo wangu! Wabarikiwe Waasuri walio kazi ya mikono yangu! Wabarikiwe Waisiraeli walio fungu langu, nililojipatia!
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66