bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 10
Isaiah 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 11 →
1
Yatawapata wenye hukumu wanaopotoa hukumu, nao waandishi wanaoandika makorofi!
2
Hutaka kuwazuia wanyonge, wasije shaurini, huyapokonya yawapasayo wakiwa wao walio ukoo wangu; tena hutaka, wajane wawe mateka yao, nao wafiwao na wazazi huwanyang'anya mali zao.
3
Siku ya kukaguliwa itakapofika, mtafanya nini, upepo wa kimbunga utokao mbali utakapovuma? Mtamkimbilia nani, awasaidie? Nayo matukufu yenu mtayapeleka wapi, myafiche?
4
Nanyi hamtaona mzungu kuliko huu: kupiga magoti kwenye mateka au kutupwa kwenye mizoga. Lakini kwa hayo yote makali yake hayajatulia bado, nao mkono wake ungaliko umekunjuka.
5
Yatawapata Waasuri nao, ijapo makali yangu yawatumie kuwa fimbo, ijapo machafuko yangu yawe vigongo mikononi mwao.
6
Ninawatuma kujia kabila lililojichafua, ninawaagizia watu, ambao ninawakasirikia, wateke mateka na kuyapokonya mapokonyo, wawakanyage kama matope ya njiani.
7
Lakini wenyewe hawafikiri kama hivyo, wala mioyo yao haina mawazo kama hayo, kwani mioyoni mwao mna neno moja tu: Kuangamiza! Makabila ya watu, wanayotaka kuyang'oa, si machache.
8
Kwani husema: Wakuu wetu wote pamoja sio wafalme?
9
Je? Mji wa Kalno haukuangamia kama ule wa Karkemisi? Mji wa Hamati haukuangamia kama ule wa Arpadi? Nao mji wa Samaria haukuangamia kama ule wa Damasko?
10
Kama mikono yetu ilivyowapata wafalme wa kimizimu na vinyago vyao vilivyokuwa vyenye nguvu kuliko vile vya Yerusalemu na vya Samaria,
11
je? Yale, tuliyowafanyizia Wasamaria na vinyago vyao, yaleyale tusiwafanyizie Wayerusalemu na vinyago vyao?
12
Lakini hapo, Bwana atakapokuwa ameyamaliza matendo yale mlimani kwa Sioni namo Yerusalemu, ndipo, yatakapokuwa aliyoyasema kwamba: Nitauumbua moyo wa mfalme wa Asuri kwa ajili ya uzao wa ukuu wake na kwa ajili ya utukufu wa macho yake wa kujitukuza.
13
Kwani alisema: Nikifanya hayo ni nguvu za mikono yangu, tena ni werevu wangu wa kweli, kwani mimi ni mwenye akili. Mimi nimeondoa mipaka ya makabila ya watu, nikayapokonya malimbiko yao, nikawa ng'ombe mkali, nikawakumba waliokalia viti vya kifalme.
14
Mkono wangu ukaona mali za makabila ya watu, kama wengine wanavyoona vituo vya ndege. Kama watu wanavyookota mayai yaliyoachwa, ndivyo, mimi nilivyookota nchi nzima; nako hakuwako mwenye kupanua bawa, wala mwenye kufumbua kinywa wala mwenye kulia.
15
Shoka litawezaje kujitukuza mbele yake aliyelitumia la kukatia? Au msumeno utawezaje kujikuza mbele yake aliyeutumia wa kukerezea? Ingekuwa kama kusema: Fimbo ndiyo inayompigisha aishikaye, au kama kusema: Kigongo kinamchukua asiye mti.
16
Kwa hiyo Bwana aliye Bwana Mwenye vikosi atatuma kwao wanene jambo litakalowakondesha, nako kwenye utukufu wao kutawaka maunguzo, nayo yataunguza, kama moto unavyounguza.
17
Nao mwanga wa Isiraeli utawawia moto; nao utukufu wao utageuka kuwa kama ndimi za moto; zitayaunguza maboma yao yenye mibigili na mikunju, yateketee kwa siku moja tu.
18
Hivyo atauangamiza utukufu wa misitu na wa mizabibu yao, kuanzia shinani mpaka kwenye nyama za ndani, itazimia, kama mwenye kufa anavyozimia.
19
Miti ya misitu yao itakayosalia itahesabika, mtoto ataweza kuiandika.
20
Siku ile waliosaa wa Isiraeli nao waliopona wa mlango wa Yakobo hawatajishikiza tena kwake yeye aliyewapiga, ila watajishikiza kweli kwa Bwana aliye Mtakatifu wa Isiraeli.
21
Watakaosalia kuwa sao la Yakobo ndio watakaomgeukia Mungu mwenye nguvu.
22
Ijapo wawe wengi kama mchanga wa ufukoni, wao walio ukoo wako wa Isiraeli, watakaomgeukia watakuwa sao tu; wengine angamizo lao litatimizwa, liyatokeze maamuzi yake kuwa ya kweli kabisa.
23
Kwani atakayelitimiza shauri la angamizo ni Bwana Mungu Mwenye vikosi, atavifanyiza katika nchi zote.
24
Kwa hiyo Bwana Mungu Mwenye vikosi anasema hivyo: Mlio ukoo wangu ukaao Sioni, msimwogope Mwasuri, ijapo awapige vigongo, awainulie fimbo yake na kuishika njia ya Wamisri.
25
Kwani bado kitambo kidogo ndipo, machafuko yatakapokoma, makali yangu yawageukie wao, yawamalize.
26
Bwana Mwenye vikosi anawashikia mjeledi, awapige, kama alivyowapiga Wamidiani kwenye Mwamba wa Kunguru, atawainulia nayo fimbo yake, kama alivyoiinulia Wamisri baharini.
27
Siku ile mizigo yao itaondoka mabegani kwenu, nayo miti yao ya kuwafunga itaondoka shingoni kwenu, itavunjika tu kwa unene, mtakaoupata tena.
28
Watakapokuja watapita Ayati, wavuke Migroni, wataiacha mizigo yao Mikimasi.
29
Kisha watapita katika lango la magenge, Geba wapige makambi ya kulala usiku, Warama watatetemeka, wa Gibea wa Sauli watakimbia.
30
Pigeni yowe, ninyi wa binti Galimu! Ninyi wa Laisi, sikilizeni! Nanyi wa Anatoti na mwone ukiwa!
31
Wa Madimena watatawanyika, wakaao Gebimu watakimbia.
32
Siku ya kusimama kwao kule Nobu watainyosha mikono yao, wauteke mlima wa binti Sioni nacho kilima cha Yerusalemu.
33
Bwana aliye Bwana Mwenye vikosi atakapotokea, ayakate matawi yao kwa nguvu zake zitishazo, ndipo, itakapovunjika nayo miti iliyokwenda juu sana, hiyo mirefu yenyewe itaanguka.
34
Navyo vichaka vya mwituni vitakatwa kwa vyuma vikali, mwitu wa Libanoni utaishia kwa nguvu za mwenye utukufu.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66