bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 40
Isaiah 40
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 41 →
1
*Watulizeni mioyo! Watulizeni mioyo walio ukoo wangu! Ndivyo, Mungu wenu anavyosema.
2
Wayerusalemu wapeni mioyo na kuwatangazia, ya kuwa utumishi wao wa vita umemalizika, ya kuwa manza zao, walizozikora, zimekwisha kulipwa, kwani mkono wa Bwana umewalipisha mara mbili makosa yao yote.
3
Iko sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani: Itengenezeni njia ya Bwana! Yanyosheni nyikani mapito ya Mungu wetu!
4
Vibonde vyote vifukiwe, navyo vilima vyote na vichuguu vyote vichimbuliwe! Napo palipopotoka panyoshwe, napo penye mashimo pawe njia ya sawasawa!
5
Utukufu wake Bwana upate kufunuliwa, wote wenye miili wauone pamoja! Kwani kinywa chake Bwana kimevisema.
6
Iko sauti ya mtu asemaye: Tangaza! Mwingine akasema: Na nitangaze nini? Kila mwenye mwili ni kama majani, nao uzuri wake wote ni kama ua la shambaani.
7
Majani hunyauka, nayo maua hupukutika, upepo wa Bwana ukiyapuzia; kweli watu ndio majani.
8
Majani hunyauka, nayo maua hupukutika, lakini Neno lake Mungu wetu litasimama kale na kale.*
9
Jipandie mlima mrefu, Sioni, upige mbiu njema! Paza sauti na nguvu, Yerusalemu, upige mbiu njema! Paza sauti, usiogope! Iambie miji ya Yuda: Mtazameni Mungu wenu!
10
Tazameni! Bwana Mungu anakuja mwenye nguvu! Mkono wake unamtengenezea ufalme. Tazama! Mshahara wake wa kulipa anao. nayo mapato yake yako mbele yake.
11
Kama mchungaji anavyolichunga kundi lake, atawakusanya wana kondoo kwa mkono wake, awabebe kifuani, nao wanyonyeshao atawapeleka polepole.
12
Yuko nani apimaye bahari kwa kofi lake? Yuko nani azilinganyaye mbingu kwa upana wa shibiri? Yuko nani aenezaye mavumbi ya nchi katika kibaba? Yuko nani apimaye milima kwa mizani au vilima kwa kipimo gani kingine?
13
Yuko nani aielekezaye roho yake Bwana? Yuko nani aliyekula njama naye ya kumjulisha jambo?
14
Yuko nani aliyepiga shauri naye la kumtambulisha kitu? Yuko nani aliyemfundisha mapito yaendayo sawasawa? Yuko nani aliyemfundisha kupambanua njia na kumjulisha utambuzi?
15
Tazameni: mataifa mazima huwaziwa kuwa kama tone la maji katika ndoo, au kama kivumbi katika mizani! Tazameni: visiwa ni kama kichanga alichokiokota!
16
Misitu ya Libanoni haitoshi kuwa kuni, nao nyama wake hawatoshi kuwa ng'ombe za tambiko.
17
Mataifa yote yako mbele yake, kama si kitu, huwaziwa kuwa kama hayako kabisa na kuwa hayana maana.
18
Mungu mtamfananisha na nani? Mtatengeneza mfano gani wa kuwa, kama yeye alivyo?
19
Labda kinyago? Tena ni fundi aliyekiumba, kisha mfua dhahabu anakifunika chote kwa dhahabu, akakitia vinyororo vya fedha.
20
Akosaye mali za kununua kipaji kama hicho huchagua mti usiooza, kisha hutafuta fundi aijuaye kazi hiyo, amsimamishie kinyago kisichoyumbayumba.
21
Nanyi hamvijui? Hamvisikii? Hamkuambiwa tangu mwanzo? Hamkuitambua misingi ya nchi?
22
Anakaa juu ya mviringo wa nchi, waikaliao wakawa kama funutu machoni pake; anazitanda mbingu kama nguo nyembamba, anaziwamba kuwa kama mahema ya kukaa. Wakuu anawatangua, wawe kama si kitu;
23
Waamuzi wa nchi nao anawatendea, kama hawana maana.
24
Wanapokuwa hawajapandwa, wala mbegu zao hazijamwagwa. wanapokuwa mashina yao hayajatia mizizi: mara anawapuzia, wakanyauka, kisha upepo mkali ukawachukua kama makapi.
25
Kwa hiyo mtanifananisha na nani, niwe, kama yeye alivyo? Ndivyo, Mtakatifu anavyosema.
26
*Yaelekezeni macho yenu juu, mtazame! Ni nani aliyeviumba hivi? Ni yeye anayevitokeza vikosi vyao hivyo, alivyovihesabu, navyo vyote pia anaviita majina. Kwa kuwa uwezo wake unazidi, nazo nguvu zake zinakaza, hakuna hata kimoja kinachokoseka.
27
Mbona unasema, Yakobo, unanena, Isiraeli: Njia yangu imefichika, Bwana asiione, nayo maamuzi, ninayoyangojea, yamempita Mungu wangu?
28
Hujayajua bado, hujayasikia bado? Mungu wa kale na kale ni Bwana aliyeyaumba mapeo ya nchi; hachoki, wala halegei, utambuzi wake hauchunguziki.
29
Achokaye humpa nguvu, asiyeweza humwongezea uwezo;
30
ijapo vijana wachoke na kulegea, ijapo wavulana nao wajikwae,
31
lakini wamngojeao Bwana hupata nguvu mpya, waruke, kama watatumia mabawa ya kozi, hupiga mbio pasipo kulegea, hukaza mwendo pasipo kuchoka.*
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 41 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66