bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 49
Isaiah 49
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 48
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 50 →
1
Nisikieni, ninyi visiwa, nanyi makabila ya watu mlioko mbali, tegeni masikio! Bwana aliniita hapo nilipozaliwa, akalikuza jina langu tangu hapo, nilipotoka tumboni mwa mama.
2
Akakitumikisha kinywa changu kama upanga mkali, akanificha kivulini mwa mkono wake, akanitumia kuwa mshale umetukao, akanificha katika podo lake.
3
Akaniambia: Ndiwe mtumishi wangu, wewe Isiraeli ndiwe, ambaye nitajitukuzia.
4
Nami nalisema: Nimejichokesha bure, nikizimaliza nguvu zangu na kusumbukia mambo yasiyo na maana, yasiyo kitu. Lakini yanipasayo yako na Bwana, mapato yangu yako na Mungu wangu.
5
Sasa nimeambiwa neno na Bwana aliyenitengeneza tumboni mwa mama kuwa mtumishi wake wa kumrudisha Yakobo kwake, Waisiraeli wapate kukusanyika kwake; kwani nimetukuka machoni pa Bwana, Mungu wangu akawa nguvu zangu.
6
Amesema hivi: Haitoshi, ukiwa mtumishi wangu wa kuiinua milango ya Yakobo na wa kuwarudisha Waisiraeli waliookoka, nimekuweka tena kuwa mwanga wa wamizimu, wokovu wangu ufike mapeoni kwa nchi.
7
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana aliyemkomboa Isiraeli, ndivyo, Mtakatifu wake anavyomwambia yeye, watu wanayembeza na kumchukia mioyoni mwao, aliye mtumishi wao wanaoitawala nchi: Wafalme watayaona, nao wakuu watainuka, wakuangukie, kwa kuwa Bwana ni mtegemevu, kwa kuwa ndiye Mtakatifu wa Isiraeli aliyekuchagua.
8
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nimekuitikia, siku zilipokuwa za kupendezwa, nikakusaidia siku ya wokovu, nikulinde, nikuweke kuwa agano lao walio ukoo wangu, uichipuze nchi, uwagawie wenyewe mafungu yao yaliyokufa,
9
uwaambie wafungwa: Tokeni! nao waliomo gizani: Kesheni! Watalisha njiani, napo vilimani po pote palipokuwa pakavu wataona malisho yao.
10
Hawataona tena njaa wala kiu, hawatapigwa na upepo wenye joto wala na jua, kwani awahurumiaye atawaongoza, awapeleke kwenye visima vya maji.
11
Nayo milima yangu yote nitaiweka kuwa njia, nazo barabara zangu zitapitia juu.
12
Na mwaone watakaotoka mbali: wengine watatoka upande wa kaskazini, wengine upande wa baharini, wengine nchi ya Sinimu.
13
Shangilieni mbingu! Nawe nchi, piga vigelegele! Nayo milima na ipige shangwe! Kwani Bwana amewatuliza walio ukoo wake, akawahurumia wanyonge walio wake.
14
Sioni ulisema: Bwana ameniacha; Bwana wangu amenisahau.
15
Je? Mwanamke humsahau mtoto wake mnyonyaji, asimhurumie mwana, aliyemzaa? Ijapo amsahau, mimi sitakusahau kamwe.
16
Tazama! Nimekuchora maganjani mwangu, kuta zako haziondoki machoni pangu.
17
Wanao wa kiume wanakuja na kupiga mbio, lakini wao waliokuvunja na kukubomoa watakutoka.
18
Yainue macho yako na kuyazungusha, uone! Hawa wote wamekusanyika, wafike kwako! Ndivyo, asemavyo Bwana: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, hawa wote utawavaa kama mapambo, utawatumia kuwa kama ukanda wa mchumba mke.
19
Kwani mahame na mapori yako na mashamba yako yaliyokufa sasa hayatawaeneza watakaokuja, wakae, nao waliokumeza watakuwa wamekwenda mbali.
20
Itakuwa, wanao waliozaliwa katika ukiwa wako wasemeane masikioni mwako: Pangu ni padogo, sogeza, ndugu yangu, nipate kukaa!
21
Nawe utasema moyoni mwako: Ni nani aliyenizalia hawa? Mimi nilikuwa sina watoto, maana nilikuwa mgumba, nilikuwa nimetekwa, nikapelekwa mbali. Basi, ni nani aliyewakuza hawa, nilipokuwa nimesazwa peke yangu? Wanatoka wapi hawa?
22
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Tazama! Nitawapungia wamizimu kwa mkono wangu, nitawatwekea makabila ya watu bendera yangu; ndipo, watakapowaleta wanao na kuwabeba vifuani, nao watoto wako wa kike watawachukua mabegani.
23
Wafalme watakuwa walezi wako, nao wake wa kifalme watakuwa wanyonyeshaji wako, watakuangukia kifudifudi, walambe mavumbi miguuni pako; ndipo, utakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, ya kuwa hawapatwi na soni waningojeao.
24
Je? Mwenye nguvu atachukuliwa mateka yake? Au kole zake mwongofu zitakombolewa?
25
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kweli nazo kole za mwenye nguvu zitachukuliwa, nayo mateka ya mkorofi yatapona; maana wao waliokugombeza nitawagombeza mimi, nao wanao nitawaokoa mimi.
26
Waliokutesa nitawalisha nyama zao, wanywe damu zao kama ni pombe, mpaka walewe; ndipo, wote wenye miili ya kimtu watakapojua, ya kuwa mimi ndimi Bwana, mwokozi wako, ni mkombozi wako akutawalaye, Yakobo.
← Chapter 48
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 50 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66