bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 28
Isaiah 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 29 →
1
Yatakupata wewe, uliye kilemba chenye majivuno ya walevi wa Efuraimu! Uliye hata sasa urembo wenye utukufu, utakuwa kama ua lililonyauka, kwa maana umejengwa kilimani juu kwenye bonde lioteshalo sana, likaalo watu waangushwao na mvinyo.
2
Tazameni! Mwenye nguvu na ukorofi yuko tayari kwa Bwana, anafanana na mvua ya mawe inayokuja na upepo unaovunjavunja, ni mvua inyeshayo maji mengi yenye nguvu ya kufurikia nchini, nayo yatawabwaga chini na kuwadidimiza kwa kuwavuta kwa nguvu zilizo kama za mkono.
3
Kisha utakanyagwa na miguu, wewe uliye kilemba chenye majivuno ya Efuraimu.
4
Lile ua litakalonyauka lingaliko, nao urembo wenye utukufu wake linao, kwa maana liko kilimani juu kwenye bonde lioteshalo sana, lakini litakuwa kama kuyu inayoiva upesi, siku za mavuno zinapokuwa hazijatimia bado; mtu akiiona anaichuma hapohapo, tena ikiwa ingalimo mkononi mwake, amekwisha kuimeza.
5
Siku ile Bwana Mwenye vikosi atakuwa kilemba chenye urembo na pambo la kipajini lenye utukufu kwao waliosalia wa ukoo wake.
6
Naye atakayekaa kitini penye uamuzi atampa roho yenye unyofu nao wapiga vita watakaowakimbiza adui malangoni atawapa nguvu za kushinda.
7
Kumbe hao nao wanapepesuka kwa mvinyo na kuyumbayumba kwa vileo! Watambikaji na wafumbuaji wanapepesuka kwa vileo: wameshikwa na kizunguzungu kwa kunywa mvinyo, wanayumbayumba kwa vileo, wanapepesuka wakifumbua, wanatukutika wakiamua.
8
Kwani meza zote zimejaa matapiko, hakuna mahali pasipo machafu.
9
Nao husema: Yuko nani, Bwana atakayemfundisha kujua maana? Yuko nani, atakayemtambulisha waliyoyasikia? Ni wao waliozoezwa, waache kunyonya, walioondolewa sasa hivi kwenye maziwa ya wamama?
10
Agizo hufuata agizo, kweli agizo hufuata agizo; kingojeo huita kingojeo, kweli kingojeo huita kingojeo kwamba: Hapa bado kidogo napo hapo bado kidogo!
11
Ni kweli, midomo, watu wasiyoitambua, nazo ndimi zilizo ngeni kwao ndizo, atakazozitumia atakaposema nao walio wa ukoo huu.
12
Maana aliwaambia: Hapo ni penye kupumzikia, waacheni wachovu, wapumzike! Hapa ni penye kutulia! Lakini hawakutaka kusikia.
13
Kwa hiyo lile neno lao litakuwa kwao neno la Bwana: Agizo hufuata agizo, kweli agizo hufuata agizo, kingojeo huita kingojeo, kweli kingojeo huita kingojeo kwamba: Hapa bado kidogo napo hapo bado kidogo! Kusudi waende na kujikwaa na kuanguka kichalichali, wapondeke, wanaswe, watekwe.
14
Kwa hiyo lisikieni neno la Bwana, ninyi waume mfyozao, nanyi mnaowatawala wa Yerusalemu walio wa ukoo huu!
15
Kwani mlisema: Tumekwisha kuagana na kufa, nako kuzimu tumekwisha kupatana nako kwamba: Pigo la kudidimiza litakapokutia, lisitufikie! Kwani uwongo tumeutumia kuwa kimbilio letu, tukajificha kwenye madanganyifu.
16
Lakini hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitazameni! Mimi ndimi niliyeweka jiwe, liwe msingi wa Sioni, nalo ni jiwe lililojulika, ya kuwa litafaa la pembeni kwa utukufu wake, likawekwa la msingi kuwa kama mwamba, ni hili la kwamba: Alitegemeaye hatakimbia.
17
Nayo yaliyo sawa nikayatumia kuwa kamba ya kupimia, nayo yaongokayo kuwa kipimo chenyewe, mvua ya mawe italiondoa kimbilio lenu la uwongo, nalo ficho lenu maji yatalididimiza.
18
Nayo mliyoyaagana na kufa yatatanguliwa, yasisimamike mliyoyapatana na kuzimu; pigo la kudidimiza litakapotukia, ndipo, watakapopokonywa nalo.
19
Kila mara litakapopita litawashika, kila kunapokucha litapita, hata mchana na usiku; nako kustushwa ndiko peke yake kutakakowatambulisha mliyoyasikia.
20
Kwani: Kitanda kifupi, hutaweza kujinyosha; nalo: Blanketi dogo, hutaweza kujifunika.
21
Kwani Bwana atainuka kama kwenye mlima wa Perasimu, achafuke kama kule bondeni karibu ya Gibeoni, aifanye kazi yake, nayo hiyo kazi yake ni ngeni, atumike katika matumishi yake, nayo hayo matumishi yake hayajasikiwa bado.
22
Sasa acheni kufyoza, vifungo vyenu visikazwe, kwani nchi zote zimekwisha kukatiwa shauri la angamizo, kama nilivyosikia kwa Bwana Mungu aliye Mwenye vikosi.
23
Sikilizeni, mwisikie sauti yangu! Angalieni, mlisikie neno langu!
24
Inakuwaje? Mlima hulima siku zote, apate kumwaga mbegu? Au huponda siku zote madongo na kupalinganya?
25
Au sivyo: alipokwisha kuusawasawisha mchanga wa juu, humwaga mbegu za maboga na za pilipili, nazo huzitupatupa, kisha hupanda nazo ngano nzuri mistarimistari, hata mtama na mahindi, nao uwele kandokando?
26
Hivyo Mungu wake alimfundisha yafaayo na kumwonyesha.
27
Kwani mbegu za maboga hazipurwi kwa magogo, mbegu za pilipili hazipitwi juu na magurudumu ya magari, ila mbegu za maboga zinafikichwa kwa vijiti, pilipili vilevile zinapigwapigwa kwa fimbo.
28
Je? Ngano zinapondwa? Hapana, hawazipuri pasipo kukoma; hata wakipitisha magari na farasi wao, hawazipondi.
29
Hayo nayo yalitoka kwake Bwana Mwenye vikosi, mizungu yake hustaajabisha, utambuzi wake ni mkuu.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66