bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Isaiah 3
Isaiah 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 4 →
1
Mtaona, Bwana aliye Bwana Mwenye vikosi akiondoa katika Yerusalemu na katika Yuda yote yatumikayo kuwa shikizo: kila shikizo la vilaji na kila shikizo la maji;
2
wenye nguvu nao wajuao kazi za vita, waamuzi na wafumbuaji, waaguaji na wazee,
3
wakuu wa askari na wenye macheo makubwa, wakata mashauri na mafundi wa kazi na mafundi wa uganga.
4
Kisha nitawapa vijana, wawe wakuu wao, nao wenye ukorofi watawatawala;
5
nao wenyewe watatesana waume na waume wenzao, kila mtu na ndugu yake, vijana watajivuna na kuwabeza wazee, nao wanyonge watawabeza wenye utukufu.
6
Hapo itakuwa, mtu amkamate ndugu yake, ambaye alizaliwa naye nyumbani mwa baba yake, amwambie: Unazo nguo bado, sharti uwe mwamuzi wetu! Hame hili liwe mkononi mwako!
7
Naye atajibu siku ileile na kupaza sauti: Mimi si mganga! Humu nyumbani mwangu hamna mkate wala nguo, msiniweke kuwa mwamuzi wenu!
8
Kwani Yerusalemu utakuwa umejikwaa, nayo Yuda itakuwa imeanguka, kwa kuwa ndimi zao na kazi zao zilimpinga Bwana na kuyachafua macho yake yenye utukufu,
9
ukorofi wa nyuso zao ukawaumbua, nao huyasimulia makosa yao pasipo kuyaficha kwa hivyo, wanavyofanana nao Wasodomu. Roho zao zitalipizwa vibaya, walivyojifanyizia wenyewe.
10
Yawazeni, ya kuwa waongofu huona mema, kwani huyala mapato ya kazi zao!
11
Lakini wasiomcha Mungu huona mabaya, kwani mikono yao iliyoyafanya, watafanyiziwa nao.
12
Wanaowasonga walio ukoo wangu ni watoto, nao wanawake ndio wanaowatawala. Ninyi mlio ukoo wangu, viongozi wenu huwapoteza, nazo njia zenu zilizowapasa kuzishika huzifisha.
13
Bwana ameinuka kupigana, Bwana amesimama kuyapatiliza makabila ya watu.
14
Bwana atakuja kuwahukumu wazee na wakuu wao walio ukoo wake, kwamba: Ninyi mmeilisha mizabibu yangu! Mliyoyanyang'anya wanyonge, yamo nyumbani mwenu.
15
Imekuwaje, mkiwaponda hivyo walio ukoo wangu? Mkizirarua nyuso za wanyonge hivyo? Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu Mwenye vikosi.
16
Bwana amesema: Kwa kuwa wanawake wa Sioni wamejikuza, wakatembea na kunyosha shingo na kutupia wengine macho yenye utongozi, wakienda na kuchezacheza na kuipigapiga mikufu ya miguu yao:
17
Bwana atawauguza wanawali wa Sioni upele wa vichwani, yeye Bwana atawavua nazo nguo za kujifunika shungi.
18
Siku ile Bwana atayaondoa mapambo kwao: vikuku na mifano ya jua vipajini nayo manyamwezi shingoni,
19
mapete masikioni na mikufu mikononi na mabuibui nyusoni;
20
hata miharuma vichwani na mikufu miguuni na mikanda viunoni na vichupa vya marashi vifuani na hirizi zote miilini po pote,
21
nazo pete vidoleni na vipini puani,
22
tena nguo za sikukuu, kama marinda na kanga na vijamanda,
23
hata vioo na fulana za hariri na vilemba na kaya.
24
Hivyo penye manukato mazuri utakuwa mnuko wa kuoza, penye mikanda watapata kamba tu, penye misuko ya nywele patakuwa na vipara, penye zile nguo za urembo watajivika magunia, maumbufu matupu yatapashika mahali pa uzuri.
25
Waume wenu watauana kwa panga, vijana wenu wenye nguvu watamalizika vitani.
26
Kwa hiyo malango yake yatapiga kite kwa kusikitika, nao wenyewe watakaa uvumbini kwa kuwa peke yao tu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66